Pata taarifa kuu

Balozi wa Ufaransa nchini Poland aitishwa kujieleza kufuatia matamshi ya Macron

Balozi wa Ufaransa mjini Warsaw ameitishwa Ijumaa hii kuripoti mbele ya Wizara ya Mambo ya Nje kwa sababu ya matamshi yaliyotolewa na Emmanuel Macron dhidi ya Waziri Mkuu wa Poland, anayeshutumiwa na rais wa Ufaransa kwa "chuki kali za mrengo wa kulia dhidi ya Wayahudi".

Waziri Mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki akiwasili kwa mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya, mjini Brussels, Ubelgiji, Machi 25, 2022.
Waziri Mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki akiwasili kwa mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya, mjini Brussels, Ubelgiji, Machi 25, 2022. REUTERS - WOLFGANG RATTAY
Matangazo ya kibiashara

"Kufuatia taarifa zilizomo katika mahojiano na Rais wa Jamhuri ya Ufaransa Emmanuel Macron na Gazeti la Le Parisien, Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland Zbigniew Rau ameamua kumwitisha Balozi wa Ufaransa", msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Poland amebaini kwenye Twitter.

Matamshi haya yameuja baada ya kiongozi wa serikali nchini Poland kumshambulia kwa maneno siku ya Jumatatu kwa mazungumzo ya simu na Vladimir Putin. β€œBwana Rais Macron, umefanya mazungumzo mara ngapi na Putin, umefanikiwa nini? Hatufany mjadala, hatufanyi mazungumzo na wahalifu, wahalifu lazima wapigwe vita,” alisema Bw Morawiecki.

Matamshi ya Macron yalichukuliwa kuwa "hayaeleweki" na Waziri Mkuu wa Poland

"Hakuna mtu aliyejadiliana na Hitler. Je, ungejadiliana na Hitler, na Stalin, na Pol Pot", aliuliza Waziri Mkuu wa Poland, akiwashutumu baadhi ya viongozi wa Ulaya kwa "kuwa na kauli zisizofaa". Ijumaa hii, msemaji wa serikali ya Poland ametaja matamshi ya Rais Macron "yasiyoeleweka" na kuyahusisha na "hisia za kisiasa zinazoambatana na kila kampeni ya uchaguzi".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.