Pata taarifa kuu

Ukraine yajiandaa kwa mapigano makali Mashariki

Mashariki mwa Ukraine sasa inalengwa na mashambulizi ya Kremlin. Raia wametakiwa kukimbia mapigano yanayojiri, licha ya vikwazo vipya "vibaya" vya Marekani dhidi ya Urusi.

Wanawake waliovalia bendera ya Ukraine wakiimba nyimbo za kizalendo wakati wa maandamano ya kutaka Ulaya kuchukuwavikwazo vdhidi ya mafuta na gesi kutoka Urusi mbele ya makao makuu ya Bunge la Ujerumani, Bundestag.
Wanawake waliovalia bendera ya Ukraine wakiimba nyimbo za kizalendo wakati wa maandamano ya kutaka Ulaya kuchukuwavikwazo vdhidi ya mafuta na gesi kutoka Urusi mbele ya makao makuu ya Bunge la Ujerumani, Bundestag. AFP - JOHN MACDOUGALL
Matangazo ya kibiashara

Jumatano hii, Kyiv ilitoa wito kwa raia wake kuondoka mashariki mwa nchi kutokana na tishio la mashambulizi ya Urusi. Severodonetsk, jiji la mashariki linalodhibitiwa na jeshi la Ukraine, ndilo lililolengwa na mashambulizi ya hivi punde.

Marekani ilitangaza Jumatano kuziwekea vikwazo benki kubwa za Urusi Sberbank na Alfa Bank na binti wawili wa Vladimir Putin kufuatia ugunduzi wa miili mingi ya raia katika miji kadhaa karibu na Kyiv. Umoja wa Ulaya, kwa upande wake, bado iko kwenye majadiliano ya kuamua hatua mpya ya vikwazo, inayolenga hasa sekta ya nishati.

Katika eneo la Kyiv, ambalo jeshi la Urusi limeondoka, hofu ya ugunduzi mpya wa miili ya watu waliouawa inaongezeka baada ya mauaji ya Bucha. Ripoti mpya zimebaini kwamba maeneo kadhaa nchii Ukraine yamekumbwa na matukio mabaya zaidi.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne. Aliomba Urusi "kuwajibishwa". Hata hivyo Urusi inakanusha kuhusika katika mauaji haya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.