Pata taarifa kuu

Ukraine: Washington yaziwekea vikwazo benki mbili kubwa za Urusi na binti wa Putin

Marekani imetangaza kuziwekea vikwazo benki kubwa za Urusi Sberbank na Alfa Bank na binti wawili wa Vladimir Putin kufuatia ugunduzi wa miili mingi ya raia katika miji kadhaa karibu na Kyiv. Mauaji yanayohusishwa vikosi vya Urusi.

Benki ya Sberbank ni moja wapo ya benki kuu za Urusi zilizoathiriwa na vikwazo vipya vya Marekani vinavyohusishwa na miili mingi ya raia iliyopatikana katika mkoa wa Kyiv baada ya kuondoka kwa wanajeshi wa Urusi.
Benki ya Sberbank ni moja wapo ya benki kuu za Urusi zilizoathiriwa na vikwazo vipya vya Marekani vinavyohusishwa na miili mingi ya raia iliyopatikana katika mkoa wa Kyiv baada ya kuondoka kwa wanajeshi wa Urusi. REUTERS/Sergei Karpukhin
Matangazo ya kibiashara

Vikwazo hivyo vinafuatia ufichuzi mpya wa ukatili unaofanywa na wanajeshi wa Urusi nchini Ukraine, zikiwemo picha za miili ya raia iliopatikana katika mitaa ya Bucha, karibu na mji mkuu wa Kyiv.

Urusi inasema, bila ushahidi, picha hizo zinazonyeshwa na maafisa wa Kyiv ni feki.

Orodha hiyo pia inajumuisha familia ya Waziri wa Mambo ya Nje Sergei Lavrov na benki kuu.

Kwa upande mwingine Moscow imewaondoa wanajeshi wake kutoka Kyiv na kuelekeza mtazamo wake kwa Donbas ya zamani ya makaa ya mawe na chuma - ambayo inajumuisha mikoa miwili mikubwa ya mashariki, Luhansk na Donetsk.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.