Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Mji wa Kramatorsk wakabiliwa na tishio la Urusi

Mashambulizi kadhaa ya anga yaliukumba mji wa Kramatorsk usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne wiki hii , jiji kubwa linalodhibitiwa na Kyiv mashariki mwa Ukraine ambalo linakabiliwa na tishio la kushambuliwa na wanajeshi wa Urusi.

Familia zinaagana katika kituo cha treni cha Kramatorsk mnamo Aprili 3, 2022.
Familia zinaagana katika kituo cha treni cha Kramatorsk mnamo Aprili 3, 2022. AFP - FADEL SENNA
Matangazo ya kibiashara

Urusi inajiimarisha ili "kuchukua udhibiti wa mji wa Donbass", mashariki mwa Ukraine, na kufikia "daraja la ardhini na Crimea", lililochukuliwa na Moscow mnamo mwaka 2014, katibu mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg amesema Jumanne. "Tuko katika awamu muhimu ya vita," ameonya wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika mkesha wa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Alliance.

Wakati kampeni za kijeshi zikielekea mashariki mwa nchi hiyo, Jumanne asubuhi kulitokea mashambulizi makubwa ya anga katika eneo la Kharkiv na hata hivyo, makao makuu ya jeshi la Ukraine wanafikiri kwamba mamlaka ya Urusi itaanzisha mashambulizi dhidi ya mji wa pili wa nchi hiyo kwa ukubwa, ameripoti mwandishi wetu Stéphane Siohan. Mashambulizi ya anga  pia yameripotiwa katika mkoa wa Dnipro, katikati mwa nchi kwenye Mto Dnieper, na hofu sasa inatanda huko Mariupol, ambapo mapigano makali yanaripotiwa, huku majeshi ya Ukraine yakionekana kuelemewa na huenda mji huo ukaanguka mikononi mwa jeshi la Urusi kwa masaa machache au kwa siku chache zijazo.

Wakati huo huo nchi 27 za Umoja wa Ulaya zinajadili kuhusu vikwazo dhidi ya uagizaji wa makaa ya mawe na mafuta kutoka Urusi na mafuta, baada ya kugunduliwa kwa idadi kubwa ya miili ya watu waliouawa katika eneo la Kyiv, alisema Jumanne afisa wa Umoja wa Ulaya huko Luxembourg. "Kuna majadiliano kuhusu kile kinachoweza kufanywa katika sekta ya nishati, kama makaa ya mawe na mafuta," Kamishna wa Biashara wa Umoja wa Ulaya Valdis Dombrovskis amesema kabla ya mkutano wa mawaziri wa fedha wa Umoja wa Ulaya mjini Luxembourg kujadili maudhui ya kifurushi cha tano cha vikwazo vya Ulaya. "Kwa Tume ya Ulaya, hakika hii ni chaguo. Lakini tunahitaji kupata mwafaka kati ya nchi wanachama,” amekiri.

Hata hivyo nchi hizi Ishirini na Saba zimegawanyika katika suala la vikwazo vinavyohitaji umoja. Poland na nchi za Baltic zinashinikiza kuchukuliwa hatua kali zinazolenga sekta ya nishati ambayo ni mojawapo ya rasilimali kuu za Urusi kufadhili vita nchini Ukraine. Lakini nchi nyingine, hasa Ujerumani, lakini pia Austria, zimejizuia kutoa msimamo wao, kwa sababu ya gharama inayotokana na shughuli zao za kiuchumi hutegemea sana mafuta kutoka Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.