Pata taarifa kuu

Ukraine: Volodymyr Zelensky kujieleza mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Katika siku ya 41 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Jumanne hii Aprili 5, hasira inaendelea baada ya ugunduzi mkubwa wa miili mingi ya raia katika maeneo ambayo hapo awali yalikuwa chini ya udhibiti wa Urusi, karibu na mji wa Kyiv.

Baada ya kugunduliwa kwa miili mingi ya raia katika mji wa Bucha, karibu na Kyiv, saa chache baada ya kuondoka kwa wanajeshi wa Moscow, jumuiya ya kimataifa imelaani mauaji hayo, huku nchi kadhaa zikibaini kwamba ni "mauaji ya kimbari" .
Baada ya kugunduliwa kwa miili mingi ya raia katika mji wa Bucha, karibu na Kyiv, saa chache baada ya kuondoka kwa wanajeshi wa Moscow, jumuiya ya kimataifa imelaani mauaji hayo, huku nchi kadhaa zikibaini kwamba ni "mauaji ya kimbari" . AP - Felipe Dana
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anatarajiwa kuzungumza mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo Jumanne.

Baada ya kugunduliwa kwa miili mingi ya raia katika mji wa Bucha, karibu na Kyiv, saa chache baada ya kuondoka kwa wanajeshi wa Moscow, jumuiya ya kimataifa imelaani mauaji hayo, huku nchi kadhaa zikibaini kwamba ni "mauaji ya kimbari" na kutaka uchunguzi wa kimataifa ufanyike. Kwa upande wake, Michelle Bachelet, kamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, amema "amesikitishwa" na picha za Bucha.

Wakati huo huo Marekani na washirika wake wanatarajia  kutangaza "wiki hii" vikwazo vipya vya kiuchumi dhidi ya Urusi, huku Ukraine ikipokea msaada zaidi wa kijeshi, Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa White House Jake Sullivan alitangaza siku ya Jumatatu.

Hata hivyo Urusi imekanusha kuhusika na mauaji haya na imeomba mjadala katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili kutoa uamuzi juu ya "chochezi za chuki" zilizofanywa na Ukraine huko Bucha, kulingana Moscow.

Vikosi vya Urusi vinatayarisha "shambulio kubwa" dhidi ya wanajeshi wa Ukraine katika eneo la Lugansk mashariki mwa Ukraine, gavana mkoa huo, Serguiï Gaïdaï, alitangaza siku ya Jumatatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.