Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Kuelekea vikwazo vipya vya nchi za Magharibi dhidi ya Urusi

Katika siku ya 42 ya uvamizi wa Urusi nchino Ukraine, Aprili 6, fuata taarifa za hivi punde moja kwa moja. Nchiza Magharibi zimarisha misimamo yao Jumatano hii baada ya ugunduzi wa hivi majuzi wa maiti nyingi huko Bucha, karibu na mji mkuu wa Ukraine ambapo mashambulizi ya anga ya Urusi yanaendelea katika maeneo kadhaa muhimu ya kimkakati.

Vizuizi vya kuzuia magari makubwa ya kijeshi katikati mwa Odessa, Aprili 5, 2022.
Vizuizi vya kuzuia magari makubwa ya kijeshi katikati mwa Odessa, Aprili 5, 2022. AFP - OLEKSANDR GIMANOV
Matangazo ya kibiashara

Pointi kuu:

► Milipuko ilitokea Jumanne jioni katika mji mdogo wa Radekhiv, kilomita 70 kutoka Lviv, jiji kubwa la magharibi mwa Ukraine, ametangaza afisa wa eneo hilo, akitoa wito kwa raia kutotroka nje hovyo.

► Baada ya kugunduliwa kwa miili mingi ya raia katika jiji la Bucha, karibu wanadiplomasia 200 wa Urusi wamefukuzwa kutoka Ulaya katika muda wa saa 48 zilizopita. Na mataifa yenye nguvu ya Magharibi - Marekani kwa uratibu na Umoja wa Ulaya (EU) na nchi zilizostawi kiviwanda (G7) - zinajiandaa kuiwekea Urusi vikwazo vipya.

►Marekani ilitangaza Jumanne kwamba itatoa msaada wa ziada wa usalama kwa Ukraine wa hadi dola milioni 100 ili kukabiliana na uvamizi wa Urusi.

► Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alizungumza Jumanne mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Alidai mbele ya Umoja wa Mataifa kwamba Urusi "iwajibishwe" kwa "uhalifu mbaya zaidi wa kivita" tangu Vita vya Pili vya Dunia, kulingana na yeye. Urusi imekanusha kuhusika kwa dhulma hizi na imeomba mjadala katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutoa uamuzi juu ya "chokozi za chuki" zilizofanywa na Ukraine huko Bucha, kulingana na Moscow.

► Urusi inajiimarisha ili "kuchukua udhibiti wa Donbass nzima", mashariki mwa Ukraine, na kufikia "daraja la ardhini na Crimea", lililochukuliwa na Moscow mnamo mwaka 2014, katibu mkuu wa  NATO, Jens Stoltenberg alisema Jumanne wiki hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.