Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Zelensky ahimiza Umoja wa Mataifa kuchukua hatua

Katika siku ya 41 ya uvamizi wa Urusi nchini UkraineJumanne hii Aprili 5, hasira inaendelea baada ya ugunduzi mkubwa wa miili mingi ya raia katika maeneo ambayo hapo awali yalitekwa na Urusi, karibu na mji wa Kyiv.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) kwa njia ya video mnamo Aprili 05, 2022 huko New York.
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky akihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) kwa njia ya video mnamo Aprili 05, 2022 huko New York. © Spencer Platt/Getty Images/AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amelihutubia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne. Tangu jana usiku, Kramatorsk mashariki mwa Ukraine imekuwa chini ya tishio la mashambulizi ya wanajeshi wa Urusi.

Rais Zelensky ameitaka Urusi "kuchukuliwa hatua", akisema inapaswa kufikishwa mbele ya mahakama ya kimataifa sawa na ile iliyofanyika Nuremberg baada ya Vita vya Pili vya Dunia.

"Mauaji" huko Bucha ni mfano mmoja tu wa mengi ya yale ambayo Urusi imekuwa ikifanya katika siku 41 zilizopita, Zelensky amesema.

Bw. Zelensky pia amehoji jukumu la Urusi ndani ya Umoja wa Mataifa, akisema uvamizi huo "unadhoofisha" usalama wa kimataifa.

Ametoa wito kwa baraza hilo kuiondoa Urusi kama mwanachama wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.