Pata taarifa kuu
UFARANSA-UCHAGUZI

Anne Hidalgo anadi sera zake kuelekea uchaguzi wa urais Ufaransa

Mgombea urais nchini Ufaransa kupitia chama cha Kisosholisti Anne Hidalgo ambaye pia ni Meya wa jiji la Paris, anaahidi mabadiliko iwapo atachuguliwa kuwa rais Aprili 10.

Mgombea urais nchini Ufaransa kupitia chama cha Kisosholisti Anne Hidalgo.
Mgombea urais nchini Ufaransa kupitia chama cha Kisosholisti Anne Hidalgo. © RFI
Matangazo ya kibiashara

Akiendelea na kampeni zake, Kaskazini mwa Ufaransa, Hidalgo amewaambia wafuasi wake, na wale wanaoamini katika sias aza Kisosholisti, kuwa, chala hicho hakifa kama wapinzani wake wanavyodai.

Aidha, amesema iwapo atashinda, atahakikisha kuwa anatekeleza mawazo ya chama hicho ambacho kiliwahi kumletea madarakni aliyekuwa rais Francois Hollande.

Amewahikishia wafausi wake kuwa, hata iwapo hatofanikiwa kuingia Ikulu, chama hicho hakitokufa kama ambavyo wapinzani wake wanavyotabiri.

Mgombea mwanamke, Marine Le Pen anaye ameendelea na kampeni zake huku wafuasi wake wakimpa hakikisho uwa wamechoshwa na rais Emmanuel Macron anayesaka muhula wa pili.

Jana Macron alimshambulia kwa maneno mpinzani wake kisiasa, Marine Le Pen, baada ya kuwataka wafuasi wake kutodharau chochote kitakachosemwa, wakato huu kura za maoni zikionesha kuwa wagombea hao wakuu wakikaribiana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.