Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Zelensky atoa wito wa vikwazo vikali dhidi ya Urusi

Katika siku ya 34 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Jumanne hii, Machi 29, mazungumzo yanafunguliwa mjini Istanbul, huku Volodymyr Zelensky akitoa wito wa kuwekewa vikwazo zaidi dhidi ya Urusi. Mamlaka ya Ukraine inadai kuwa imerejesha himaya yake katika mji wa Irpin lakini hali inatia wasiwasi huko Mariupol, ambapo takriban watu 5,000 wanasemekana kufariki.

Mwanajeshi wa Ukraine akipita kwenye mitambo ya lijeshi akiwa amesimama katika ulinzi kwenye kituo cha ukaguzi nje kidogo ya jiji la Kyiv mnamo Machi 28, 2022.
Mwanajeshi wa Ukraine akipita kwenye mitambo ya lijeshi akiwa amesimama katika ulinzi kwenye kituo cha ukaguzi nje kidogo ya jiji la Kyiv mnamo Machi 28, 2022. AFP - SERGEI SUPINSKY
Matangazo ya kibiashara

Pointi kuu:

► Takriban watu 5,000 wamefariki dunia huko Mariupol, jiji lililozingirwa na Urusi kwa wiki kadhaa, kulingana na afisa wa Ukraine. Umoja wa Mataifa unatafuta kufikiwa kwa "maelewano ya kusitisha mapigano" ili kuruhusu misaada kufafiki walengwa.

► Mamlaka nchini Ukraine ilisema siku ya Jumatatu kwamba vikosi vyake vimeuteka mji wa Irpin, katika vitongoji vya Kyiv. Vikosi vya Ukraine pia vimezuia mashambulizi ya Urusi kuelekea Brovary, mashariki mwa Kyiv, katika muda wa saa 24 zilizopita.

► Katika mikoa ya Chernigiv, Sumy, Kharkiv, Donbass, na kusini mwa Ukraine "hali inaendelea kuwa ya wasiwasi", alitangaza Jumatatu jioni rais wa Ukraine.

► Mamluki wa Urusi kutoka kundi la Wagner wametumwa mashariki mwa Ukraine, Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema Jumatatu, ambayo inakadiria kuwa zaidi ya wapiganaji 1,000 kutoka kwa kampuni ya mamluki ya Wagner wanaweza kuletwa kupigana nchini humo.

►Duru mpya ya mazungumzo inatarajiwa kufanyika Jumanne hii mjini Istanbul, kulingana na picha kutoka kituo cha televisheni cha Uturuki NTV. Pande zote mbili zilisema Jumatatu hazitarajii mafanikio makubwa katika mazungumzo hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.