Pata taarifa kuu

Watu 5,000 wauawa Mariupol, Umoja wa Mataifa wataka "kusitishwa kwa mapigano"

Katika siku ya 33 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, mazungumzo mapya yanafunguliwa nchini Uturuki huku Zelensky akisema anathmini "kwa kina" suala la "kutoegemea" kwa Ukraine na mamlaka imekataa kuwaondoa raia leo kwa hofu ya "chokochoko za Urusi".

Waokoaji katika eneo la hospitali ya wanawake huko Mariupol, iliyokumbwa na mashambulizi ya jeshi la Urusi mnamo Machi 9, 2022.
Waokoaji katika eneo la hospitali ya wanawake huko Mariupol, iliyokumbwa na mashambulizi ya jeshi la Urusi mnamo Machi 9, 2022. AP - Evgeniy Maloletka
Matangazo ya kibiashara

Pointi kuu:

Wajumbe wa Urusi na Ukraine walithibitisha Jumapili kwamba duru mpya ya mazungumzo itafanyika mwanzoni mwa juma hili. Kwa mujibu wa Kyiv, mazungumzo haya ya ana kwa ana yatafanyika kuanzia Jumatatu Machi 28 hadi Jumatano Machi 30 nchini Uturuki, wakati mpatanishi mkuu wa Urusi ametaja tarehe za Jumanne na Jumatano, bila kutaja eneo ambapo mazungumeo hayo yatafanyika. Pande zote mbili zimesema Jumatatu hazitarajii maendeleo makubwa kutoka kwa mazungumzo hayo.

► Takriban watu 5,000 waliuawa huko Mariupol, jiji lililozingirwa na Urusi kwa wiki kadhaa, kulingana na afisa wa Ukraine. Mapigano yanaripotiwa karibu na Kyiv.

► Rais wa Ukraine Voldymyr Zelensky alisema katika mahojiano na vyombo vya habari huru vya Urusi siku ya Jumapili kwamba serikali yake inachunguza "kwa kina" swali la "kutounga mkono upande wowote" kwa Ukraine. Hili ni moja ya matakwa kuu ya Moscow katika mazungumzo ya kumaliza mzozo huo.

► Milipuko mikubwa ilisikika huko Kyiv, Lutsk, Kharkiv na Zhytomyr, huku maonyo ya mashambulizi ya anga yakisikika katika takriban mikoa yote ya Ukraine siku ya Jumapili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.