Pata taarifa kuu

Ukraine: Hakuna zoezi la kuhamisha raia kwa kuogopa "chokochoko" za Urusi

Katika siku ya 33 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, mazungumzo mapya yanafunguliwa nchini Uturuki, huku Zelensky akisema anatathmini "kwa kina" swali la "kutounga mkono upande wowote" kwa Ukraine na mamlaka ya Ukraine inakataa kuwaondoa raia leo kwa hofu ya "chokochoko za Urusi".

Wanajeshi wa Jamhuri ya Watu wa Donetsk wakikagua gari katika kituo cha ukaguzi nje kidogo ya Mariupol, Ukraine, Jumapili, Machi 27, 2022.
Wanajeshi wa Jamhuri ya Watu wa Donetsk wakikagua gari katika kituo cha ukaguzi nje kidogo ya Mariupol, Ukraine, Jumapili, Machi 27, 2022. AP - Alexei Alexandrov
Matangazo ya kibiashara

Pointi kuu:

β–ΊWajumbe wa Urusi na Ukraine walithibitisha Jumapili kwamba duru mpya ya mazungumzo itafanyika mwanzoni mwa juma hili. Kwa mujibu wa Kyiv, mazungumzo haya ya ana kwa ana yatafanyika kuanzia Jumatatu Machi 28 hadi Jumatano Machi 30 nchini Uturuki, wakati mpatanishi mkuu wa Urusi ametaja tarehe za Jumanne na Jumatano, bila kutaja eneo ambapo mazungumeo hayo yatafanyika. Pande zote mbili zimesema Jumatatu hazitarajii maendeleo makubwa kutoka kwa mazungumzo hayo.

β–ΊKiev imesitisa utaratibu wa kutoa maeneo salama ya kiutu kwa kuwahamisha raia siku ya Jumatatu, kwa kuhofia "chokochoko" za Urusi.

β–Ί Rais wa Ukraine Voldymyr Zelensky alisema katika mahojiano na vyombo vya habari huru vya Urusi siku ya Jumapili kwamba serikali yake inachunguza "kwa kina" swali la "kutounga mkono upande wowote" kwa Ukraine. Hili ni moja ya matakwa kuu ya Moscow katika mazungumzo ya kumaliza mzozo huo.

β–Ί Milipuko mikubwa ilisikika huko Kyiv, Lutsk, Kharkiv na Zhytomyr, huku maonyo ya mashambulizi ya anga yakisikika katika takriban mikoa yote ya Ukraine siku ya Jumapili.

Jumla ya watu wanaojaribu kutoroka mapigano yaliyoanzishwa na jeshi la Urusi mnamo Februari 24 ni karibu milioni 3.9, kulingana na hesabu ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leoJumatatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.