Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Jeshi la Urusi kujikita mashariki mwa nchi

Katika siku ya 30 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, nchi za Magharibi zakubaliana kupunguza utegemezi wa Ulaya kwa gesi na mafuta kutoka Urusi. Rais wa Marekani Joe Biden amewasili nchini Poland. Watoto milioni 4.3 wa Ukraine wamekimbia makazi yao na jeshi la Urusi linakiri kuuawa kwa wanajeshi 1,351 katika safu yake.

Jeshi la Urusi limekiri kupoteza wanajeshi 1,351 tangu kuanza kwa vita  nchini Ukraine mwezi mmoja uliopita.
Jeshi la Urusi limekiri kupoteza wanajeshi 1,351 tangu kuanza kwa vita nchini Ukraine mwezi mmoja uliopita. REUTERS - ALEXANDER ERMOCHENKO
Matangazo ya kibiashara

Pointi kuu:

► Urusi imetangaza Ijumaa wiki hii uamuzi wake wa kujikita katika "ukombozi wa Donbass", mashariki mwa Ukraine, huku mzozo huo, ambao uko katika siku yake ya 30, ukikwama na hakuna matokeo ya wazi yanayotokea.

► Rais wa Marekani Joe Biden amewasili Poland, hatua ya pili baada ya Brussels ya ziara ya Ulaya iliyonuia kuimarisha umoja wa nchi za Magharibi dhidi ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, katika nyanja ya kidiplomasia na kiuchumi.

► Makubaliano kati ya Umoja wa Ulaya na Marekani yanafaa kutiwa saini ili kuruhusu Wamarekani kusambaza gesi asilia iliyoyeyushwa zaidi kwa Umoja wa Ulaya. Ujerumani itaweza kufanya hivyo bila makaa ya mawe kutoka Urusi.

► Jeshi la Urusi limekiri kupoteza wanajeshi 1,351 tangu kuanza kwa vita  nchini Ukraine mwezi mmoja uliopita.

► Zaidi ya nusu ya watoto wa Ukraine wamekimbia makazi yao baada ya mwezi mmoja wa vita, yaani watoto milioni 4.3, na raia milioni 10 wa Ukraine wamekimbia makazi yao kulingana na Umoja wa Mataifa.

► Hali katika jiji lililozingirwa la Mariupol, kusini mwa nchi, kwenye Bahari ya Azov, inazidi kuwa mbaya, Waukraine wanashutumu idadi kubwa ya wakazi wa mji huo kwenda Urusi. Hlamshauri ya Manispaa ya jiji inakadiria kuwa karibu watu 300 walikufa katika shambulio la bomu dhii ya ukumbi wa michezo.

Wakati huo huo Urusi kupitia msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov, imesema kuwa hakuna cha kutisha kitakachotokea iwapo Marekani na washirika wake watafanikiwa kuifukuza Urusi kutoka kundi la mataifa 20 makubwa kuichumi duniani, kwa sababu mengi ya mataifa hayo yamo kwenye vita vya kiuchumi na Moscow.

Awali Rais wa Marekani Joe Biden alisema anapendelea kuiondoa Urusi kutoka kundi la mataifa yenye uchumi mkubwa wa G20 kutokana na uvamizi nchini Ukraine. 

Peskov alisema dunia ni kubwa zaidi ya Marekani na Ulaya na kutabiri kuwa juhudi za kuitenga Moscow zitafeli.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.