Pata taarifa kuu

Biden: Marekani itachukua hatua iwapo Urusi itatumia silaha za kemikali Ukraine

Rais wa Marekani Joe Biden amesema mwanzake wa Urusi Vladimir Putin ameshindwa kuyagawa mataifa ya Magharibi, baada ya kuivamia Ukraine.

Rais Joe Biden anazungumza kuhusu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine wakati wa mkutano na waandishi wa habari baada ya mkutano wa kilele wa NATO na mkutano wa Kundi la G7 katika makao makuu ya NATO, Alhamisi, Machi 24, 2022, huko Brussels.
Rais Joe Biden anazungumza kuhusu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine wakati wa mkutano na waandishi wa habari baada ya mkutano wa kilele wa NATO na mkutano wa Kundi la G7 katika makao makuu ya NATO, Alhamisi, Machi 24, 2022, huko Brussels. AP - Evan Vucci
Matangazo ya kibiashara

Biden ametoa kauli hiyo jijini Brussels baada ya kikao cha Jumuiya ya nchi zinazounda jeshi la kujihami NATO, huku akiongeza kuwa Marekani itachukua hatua iwapo Urusi itaamua kutumia silaha za kemikali nchini Ukraine.

Viongozi wa mataifa ya Magharibi waliokutana katika kikao cha NATO, Umoja wa Ulaya na G7, wamesisitiza umuhimu wa kuungana na kuisaidia Ukraine kijeshi, huku wakikubaliana kuimarisha ulinzi zaidi Mashariki mwa bara la Ulaya.

Aidha, viongozi wa G7 wameunga mkono hatua iliyochukuliwa na Mahakama ya Kimataifa ya ICC, kuichunguza Urusi kuhusu uhusika wake wa kutekeleza uhalifu dhidi ya binadamu nchini Ukraine, ambayo imeendelea kushuhudia mashambulio yanayosababisha maafa na wakimbizi wengi zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.