Pata taarifa kuu

Warusi wakusanyika kwenye mpaka kati ya Mexico na Marekani

Vita vya Ukraine vinatikisa Ulaya na kusababisha mamilioni ya watu kuyahama makazi yao. Tangu kuanza kwa mzozo huo, Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi, UNHCR,  limehesabu zaidi ya Waukreni milioni 3.5 ambao wameikimbia nchi yao.

Mwanamke huyu akiwa na mwanawe karibu na bandari ya San Ysidro kuelekea Marekani, huko Tijuana, Mexico, Alhamisi, Machi 17, 2022.
Mwanamke huyu akiwa na mwanawe karibu na bandari ya San Ysidro kuelekea Marekani, huko Tijuana, Mexico, Alhamisi, Machi 17, 2022. AP - Gregory Bull
Matangazo ya kibiashara

Warusi pia wanatoroka nchi yao kwa wingi, wakikimbia utawala wa Vladimir Putin. Wengine, hata hivyo, hawabaki Ulaya na wameamua kwenda mbali zaidi. Ni maelfu kadhaa ambao wamewasili Mexico na mpaka wa kaskazini na Marekani.

Wanawasili katika nchi hizo kama watalii waliosafiri kwa ndege. Safari nyingi za ndege huwawezesha kuingia katika mji ya Mexico na Cancun kutoka Urusi kupitia Uturuki au Rasi ya Arabia. Hawahitaji visa kuingia Mexico na wanaweza kukaa miezi sita. Kutoka hapo, mpaka wa Marekani, hasa huko Tijuana, wanaingia kwa urahisi.

Ni vigumu kujua ni Warusi wangapi walio nchini humo, hata hivyo ni wangapi wanakusudia kujaribu kwenda Marekani. Katika mpaka, waangalizi waliona Warusi wa kwanza wakiwasili majira ya joto mwaka uliyopita na idadi yao imeongezeka kwa kasi. Katika miezi sita, kati ya mwezi wa Agosti 2021 na mwezi wa Januari 2022, zaidi ya watu 8,600 wenye asili ya Urusi waliomba hifadhi nchini Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.