Pata taarifa kuu

Urusi na Ukraine kukutana kwa mazungumzo mapya Jumanne

Mazungumzo ya ana kwa ana kati ya wajumbe wa Ukraine na Urusi, yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumanne nchini Uturuki.

Uharibifu uliofanywa na jeshi la Urusi katika mji wa Kharkiv, Ukraine.
Uharibifu uliofanywa na jeshi la Urusi katika mji wa Kharkiv, Ukraine. AP - Felipe Dana
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, Urusi inasema hakuna uwezekano wa rais Vladimir Putin, kukutana na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy ambaye amesema nchi yake iko tayari kujadiliana na Urusi kuhusu taifa hilo kutofungamana na upande wowote.

 

 

Aidha, ameendelea kuzionyooshea kidole nchi za Ulaya kwa kuitelekeza.

Wakati hayo yakijiri, hali ya kibinadamu katika mji wa Mariupol, inaendelea kuwa mbaya, wakati huu Ukraine ikisema haina mpango wa kuondoa vikwazo vya kuwaruhusu raia waliokwama kwenye miji inayoendelea kushambuliwa, baada ya kupokea ripoti kuwa, Urusi inapanga kulenga misafara ya watu wanaotoroka.

Katika hatua nyingine, Urusi imesema itazuia raia kutoka nchi ambazo sio rafiki kama Uingereza, Marekani na chi zote za Umoja wa Ulaya kuingia katika ardhi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.