Pata taarifa kuu

Suala la "kutoegemea" ambalo Moscow yadai na kutathminiwa na Kyiv lazua wasiwasi

Mazungumzo yanatarajiwa kuanza tena mwanzoni mwa juma hili nchini Uturuki. Mazungumzo hayo huend yakafanyika Jumanne Machi 29 na Jumatano Machi 30, kulingana na upande wa Urusi. Suala la kutoegemea upande wowote kwa upande wa Ukraine, litagubika kiako hiki kipya cha mazungumzo. "Suala lenyewe linatadhminiwa kwa kina", amesema rais wa Ukraine. Lakini suala hilo linazua maswali mengi.

Rais wa Urusi Vladimir Putin na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.
Rais wa Urusi Vladimir Putin na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky. Tiziana FABI, ludovic MARIN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amesema vipaumbele katika mazungumzo kati ya Ukraine na Urusi vitakuwa uhuru na mamlaka ya mipaka ya nchi yake. Ameyasema hayo jana usiku katika ujumbe wa vidio, na kuongeza kuwa ipo fursa na haja ya mkutano wa ana kwa ana nchini Uturuki, ambako duru nyingine ya mazungumzo kati ya pande hizo mbili inatarajiwa kufanyika wiki hii.

Zelenskiy pia amewaambia waandishi huru wa Urusi jana kwamba serikali yake itazingatia kutangaza kutoegemea upande na kutoa uhakikisho wa usalama kwa Urusi, ambao utahusisha Ukraine kutokuwa na silaha za nyuklia.

Kwa upande mwingine waziri wa uchumi wa Ukraine amesema vita vya Urusi dhidi ya Ukraine vimeigharimu Ukraine dola bilioni 564.9 (sawa na euro bilioni 429.3) kufikia sasa katika uharibifu wa miundombinu, kupoteza ukuaji wa uchumi na mambo mengine.

Urusi inaendelea kusema kuwa inaendesha "operesheni maalum ya kijeshi" nchini Ukraine kwa lengo la kuipokonya silaha nchi hiyo.

Ukraine na washirika wake wa Magharibi wamesema msimamo huo ni kisingizio cha uvamizi usio na msingi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.