Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Angalau watu saba wauawa na mashambulizi huko Mykolaiv

Katika siku ya 34 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Jumanne hii, Machi 29, mazungumzo yanafunguliwa mjini Istanbul, huku Volodymyr Zelensky akitoa wito wa kuwekewa vikwazo zaidi dhidi ya Urusi. Zoezi la kuwahamisha raia limeanza tena, lakini mji wa Mykolaiv umekumbwa na mashambulizi ya anga ya jeshi la Urusi.

Katika picha hii iliyotolewa na Ofisi ya Rais wa Uturuki, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akitoa hotuba ya kuwakaribisha wajumbe wa Urusi na Ukraine kabla ya mazungumzo yao, mjini Istanbul, Uturuki, Jumanne, Machi 29, 2022.
Katika picha hii iliyotolewa na Ofisi ya Rais wa Uturuki, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan akitoa hotuba ya kuwakaribisha wajumbe wa Urusi na Ukraine kabla ya mazungumzo yao, mjini Istanbul, Uturuki, Jumanne, Machi 29, 2022. via REUTERS - MURAT CETINMUHURDAR/PPO
Matangazo ya kibiashara

Pointi kuu:

►Duru mpya ya mazungumzo inafanyika Jumanne hii mjini Istanbul. Pande zote mbili zilisema Jumatatu hazitarajii mafanikio makubwa. Wajumbe wa majadiliano kutoka Urusi na Ukraine wameanza mazungumzo leo Jumanne mjini Istanbul, wakati Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan akiwaambia kuwa maendeleo katika mazungumzo hayo yatafungua njia kwa mkutano mwengine kati ya viongozi wa nchi hizo mbili- Rais Volodymyr Zelensky na Rais Vladimir Putin.

► Takriban watu 5,000 wameuawa huko Mariupol, jiji lililozingirwa na Urusi kwa wiki kadhaa, kulingana na afisa wa Ukraine. Umoja wa Mataifa unatafuta kuanzisha maelewano ya "kusitisha mapigano".

► Mamlaka nchini Ukraine ilisema siku ya Jumatatu kwamba vikosi vyake vimeuteka mji wa Irpin, katika vitongoji vya Kyiv. Vikosi vya Ukraine pia vimezuia mashambulizi ya Urusi kuelekea Brovary, mashariki mwa Kyiv, katika muda wa saa 24 zilizopita.

► Katika mikoa ya Chernigiv, Sumy, Kharkiv, Donbass, na kusini mwa Ukraine "hali inaendelea kuwa ya wasiwasi", alitangaza Jumatatu jioni rais wa Ukraine.

► Mamluki wa Urusi kutoka kundi la Wagner wametumwa mashariki mwa Ukraine, Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema Jumatatu, ambayo inakadiria kuwa zaidi ya wapiganaji 1,000 kutoka kwa kampuni ya mamluki ya Wagner wanaweza kuletwa kupigana nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.