Pata taarifa kuu

Watu zaidi ya milioni moja na nusu waitoroka Ukraine

Zaidi ya watu milioni 1.5 tayari wameikimbia Ukraine, Umoja wa Mataifa umeonya Jumapili Machi 6. Huu ni mzozo wa wakimbizi unaokua kwa kasi zaidi barani Ulaya tangu Vita vya Pili vya Dunia.

Wakimbizi wakiwasili kutoka Ukraine huko Medyka, kwenye mpaka wa Poland, Machi 6, 2022.
Wakimbizi wakiwasili kutoka Ukraine huko Medyka, kwenye mpaka wa Poland, Machi 6, 2022. © AP Photo/Visar Kryeziu
Matangazo ya kibiashara

Idadi ya watu wanaokimbia mzozo nchini Ukraine imevuka kiwango cha watu milioni 1.5, ikiwa ni mzozo wa haraka zaidi wa wakimbizi barani Ulaya tangu Vita vya Pili vya Dunia, Umoja wa Mataifa umeonya Jumapili hii Machi 6.

“Zaidi ya wakimbizi milioni 1.5 kutoka Ukraine waliondoka nchini na kukimbilia nchi jirani katika muda wa siku kumi. Huu ni mzozo wa wakimbizi unaokua kwa kasi zaidi barani Ulaya tangu Vita vya Pili vya Dunia,” Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi, Filippo Grandi amesema kwenye Twitter.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Wakimbizi, UNHCR, liliripoti Jumamosi karibu wakimbizi milioni 1.37.

Mamlaka na Umoja wa Mataifa wanatarajia idadi hiyo ya wakimbizi kuongezeka zaidi, wakati jeshi la Urusi linaendelea na mashambulizi yake, hasa katika mji wa Kiev, mji mkuu wa Ukraine.

Mashambulizi kwenye vituo vya afya

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) mjini Geneva, ripoti za mashambulizi dhidi ya vituo vya afya nchini Ukraine zinaongezeka.

“WHO imethibitisha mashambulizi kadhaa dhidi ya vituo vya afya nchini Ukraine, na kusababisha vifo na majeruhi kadhaa. Habari zingine zinachunguzwa," mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus mesema kwenye ujumbe wa twitter Jumapili.

"Mashambulizi dhidi ya vituo vya matibabu au wahudumu wa afya yanakiuka kutoegemea upande wowote wa matibabu na ni ukiukaji wa sheria za kimataifa za kibinadamu," amesema.

Poland ndiyo nchi inayohifadhi wakimbizi wengi kutoka Ukraine, baada ya mashambulizi ya kwanza ya Urusi.

Tangu Februari 24, wakati uvamizi wa Urusi nchini Ukraine ulipoanza, watu 922,400 waliokimbia mzozo wameingia Poland, walinzi wa mpaka wa Poland wametangaza Jumapili asubuhi.

Siku moja kabla, Jumamosi, wakimbizi waliowasili nchini Poland walifikisha kiwango cha rekodi kwa wasafiri 129,000, idadi kubwa ya raia wa Ukraine, lakini pia kutoka nchi zingine kadhaa ikiwa ni pamoja na Poland, Uzbekistan, Belarus, India, Nigeria, Algeria, Morocco, Afghanistan, Pakistan, Marekani na Urusi, kulingana na chanzo hicho.

Kulingana na ripoti ya kwanza ya hali ya WHO iliyochapishwa Jumamosi jioni, watu milioni 18 wameathiriwa na mzozo nchini Ukraine.

WHO imetuma wafanyakazi kwenda Moldova, Romania na Poland ili kuongeza idadi ya wafanyakazi wake. Shirika la afya la Umoja wa Mataifa pia limekusanya wataalam wa vifaa nchini Poland kuanzisha kituo cha operesheni na kusaidia maeneo salama, ili kuwezesha utoaji wa haraka wa usaidizi kwa watu walioathirika.

Mnamo Machi 4, WHO ilisafirisha kundi lake la kwanza la vifaa vya matibabu kwenda Poland, ambavyo viliwasili Ukraine kwa nia ya nchi kavu. Msaada huu hasa unapaswa kufanya iwezekanavyo kukidhi mahitaji ya afya ya watu 150,000, ikiwa ni pamoja na watu 1,000 wanaohitaji huduma ya upasuaji.

Shehena ya pili ilikuwa njiani Jumamosi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.