Pata taarifa kuu

[Moja kwa moja] Vita nchini Ukraine: Vladimir Putin asema atafikia "malengo yake"

Katika siku ya kumi na moja ya uvamizi wa Ukraine, Jumapili Machi 6, vikosi vya Urusi vinakaribia Kiev, Odessa inahofia mashambulizi ya mabomu na Mariupol imeshindwa kuwahamisha raia wake. Katika mahojiano ya simu na Emmanuel Macron, Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema "atafikia malengo yake" nchini Ukraine, "ama kwa mazungumzo au kwa njia ya vita".

Umati wa watu unajaribu kukimbia Irpin, karibu na Kiev, iliyoshambuliwa kwa mabomu katika saa za hivi karibuni.
Umati wa watu unajaribu kukimbia Irpin, karibu na Kiev, iliyoshambuliwa kwa mabomu katika saa za hivi karibuni. AP - Emilio Morenatti
Matangazo ya kibiashara

Pointi kuu:

► Jaribio la pili la kuwahamisha raia kutoka Mariupol lilikatizwa siku ya Jumapili baada ya jaribio la kwanza kufutwa siku moja kabla kwa sababu ya kutoheshimu usitishaji mapigano. Kutekwa kwa mji huu wenye wakazi 450,000, uliyoko kwenye Bahari ya Azov,kungewezesha makutano kati ya vikosi vya Urusi vinavyokuja kutoka Crimea iliyounganishwa, ambayo tayari imechukua bandari muhimu za Berdiansk na Kherson, na vikosi vilivyotangaza kujitenga na vikosi vya rusi katika jimbo la Donbass.

► Katika mahojiano ya simu ya saa 1:45 na Emmanuel Macron, Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema "atafikia malengo yake" nchini Ukraine, "ama kwa mazungumzo au kwa njia ya vita". Amekanusha kuwa jeshi la Urusi "linalenga raia" na akahakikisha kuwa "haikuwa kwa nia yake" kushambulia vinu vya nyuklia vya Ukraine.

► Wakati jeshi la Urusi linakaribia Kiev, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema Jumapili kwamba vikosi vya Urusi vinajiandaa kushambulia mji wa Odessa, ulioko kusini mwa nchi hiyo.

► Kampuni mbili kubwa za kadi za benki duniani kote Visa na Mastercard walitangaza Jumamosi Machi 5 kwamba wamesitisha shughuli zao nchini Urusi. Kadi za benki za Visa na Mastercard za Kirusi hazitakuwa halali tena nje ya nchi, na kadi zilizotolewa nje ya nchi hazitafanya kazi tena nchini Urusi.

► Kulingana na Rais wa Urusi Vladimir Putin, vikwazo vya Magharibi "ni sawa na tangazo la vita, alisema Jumamosi, kulingana na shirika la habari la Reuters, lakini tunamshukuru Mungu kuwa bado hatujafikia hilo". Kufikia sasa, msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alikuwa ametishia kulipiza kisasi dhidi ya vikwazo hivyo, bila kutoa maelezo zaidi.

► Vyombo vya habari vingi vya Ulaya, ikiwa ni pamoja na BBC, shirika la habari la Marekani Bloomberg na shirika la Uhispania la Efe wamesimamisha kazi ya wanahabari wao wote nchini Urusi, hasa ili kuhakikisha "usalama" wao, baada ya kupitishwa kwa sheria inayotoa adhabu ya kifungo kwa jela kwa utangazaji wa "habari za uwongo kuhusu jeshi".

► Duru mpya ya mazungumzo ya Urusi na Ukraine itafanyika Jumatatu Machi 7, kulingana na mkuu wa ujumbe wa Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.