Pata taarifa kuu

Ukraine: "Mapigano makali yarindima", Putin atishia kuichukulia hatua kali Ukraine

Katika siku ya kumi na moja ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, "mapigano makali" yaliripotiwa Jumapili Machi 6 kati ya vikosi vya Urusi na jeshi la Ukraine. Rais wa Urusi ameitishia Ukraine kwamba atainyima "hadhi yake kama nchi huru", akilinganisha vikwazo vya kimataifa vinavyoikumba Urusi na "tangazo la vita".

Askari wa Ukraine huko Lugansk, Machi 5, 2022.
Askari wa Ukraine huko Lugansk, Machi 5, 2022. AFP - ANATOLII STEPANOV
Matangazo ya kibiashara

► Jeshi la Urusi lilitangaza Jumamosi alasiri kwamba lilianza tena "mashambulizi" baada ya kuahirishwa kwa zoezi la kuahamisha raia kutoka Mariupol. Manispaa ya mji wa bandari hii ya kimkakati iliishutumu Moscow kwa kutoheshimu usitishaji mapigano uliotangazwa saa chache mapema. Kutekwa kwa mji huu wenye wenyeji wapatao 450,000, uliyoko kwenye Bahari ya Azov, kungewezesha makutano kati ya vikosi vya Urusi vinavyokuja kutoka Crimea iliyounganishwa, ambayo tayari imechukua bandari muhimu za Berdiansk na Kherson, na vikosi vilivyotangaza kujitenga na vikosi vya rusi katika jimbo la Donbass.

► Kampuni mbili kubwa za kadi za benki duniani kote Visa na Mastercard walitangaza Jumamosi Machi 5 kwamba wamesitisha shughuli zao nchini Urusi. Kadi za benki za Visa na Mastercard za Kirusi hazitakuwa halali tena nje ya nchi, na kadi zilizotolewa nje ya nchi hazitafanya kazi tena nchini Urusi.

► Kulingana na Rais wa Urusi Vladimir Putin, vikwazo vya Magharibi "ni sawa na tangazo la vita, alisema Jumamosi, kulingana na shirika la habari la Reuters, lakini tunamshukuru Mungu kuwa bado hatujafikia hilo". Kufikia sasa, msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alikuwa ametishia kulipiza kisasi dhidi ya vikwazo hivyo, bila kutoa maelezo zaidi.

► Vyombo vya habari vingi vya Ulaya, ikiwa ni pamoja na BBC, shirika la habari la Marekani Bloomberg na shirika la Uhispania la Efe wamesimamisha kazi ya wanahabari wao wote nchini Urusi, hasa ili kuhakikisha "usalama" wao, baada ya kupitishwa kwa sheria inayotoa adhabu ya kifungo kwa jela kwa utangazaji wa "habari za uwongo kuhusu jeshi".

► Duru mpya ya mazungumzo ya Urusi na Ukraine itafanyika Jumatatu Machi 7, kulingana na mkuu wa ujumbe wa Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.