Pata taarifa kuu
URUSI-UKRAINE-VITA

Vita vya Urusi na Ukraine: Usitishwaji wa vita washindwa kutekelezwa

Vikosi vya Urusi vimetangaza usitishwaji wa vita ili kuruhusu raia kupata hifadhi katika maeneo salama katika miji ya Mariupol na Volnovakha nchini Ukraine.

Vita katika mji wa  Mariupol nchini Ukraine unaoendelea kushambuliwa na wanajeshi wa Urusi
Vita katika mji wa Mariupol nchini Ukraine unaoendelea kushambuliwa na wanajeshi wa Urusi via REUTERS - @AYBURLACHENKO
Matangazo ya kibiashara

Licha ya tangazo hilo la Urusi, maafisa wa Ukraine wanasema, halitekelezwi na vikosi vya Urusi havijaheshimu maelewano ya usitishwaji wa vita kwa muda, na badala yake mashambulizi yanaendelea kushuhudiwa.

Kutokana na hatua hiyo, Ukraine inasema zoezi la kuwahamisha raia katika maeneo salama, limesitishwa.

Uingereza inasema, kuna uwezekano mkubwa wa  wanajeshi wa Urusi, kuzingira miji minne ya  Kharkiv, Chernihiv, Sumy na Mariupol.

Urusi ambayo imefunga mitandoa  ya facebook na Twitter kwa madai ya kusambaza habari za uongo, kupitia kwa Waziri wake wa Mambo ya nje Sergei Lavrov, amesema matamshi yanayotolewa na ungozi wa Ukraine, yanatilia shaka iwapo kuna uwezekano wa pande hizo mbili kupata mwafaka.

Wakati hayo yakijiri, Umoja wa Mataifa unasema, watu 351 wamepoteza maisha huku wengine  Milioni 1.2 wakikimbia  Ukraine, kwenda katika mataifa jirani.

Tume ya Umoja huo inayohusika na wakimbizi inasema hali nchini Ukraine inaendelea kuwa mbaya na kufikia siku ya Jumapili, idadi ya wakimbizi itakuwa imefikia Milioni 1 nukta 5.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.