Pata taarifa kuu

Ukraine: Pande mbili zatangaza usitishaji vita Mariupol ili kuhamisha raia

Katika siku ya kumi na moja ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, "mapigano makali" yameripotiwa Jumapili Machi 6 kati ya vikosi vya Urusi na jeshi la Ukraine. Rais wa Urusi ameitishia Ukraine kwamba atainyima "hadhi yake kama nchi huru", akilinganisha vikwazo vya kimataifa vinavyoikumba Urusi na "tangazo la vita".

Mtu huyu aliyejeruhiwa anapelekwa hospitalini baada ya shambulio la bomu Machi 3, 2022.
Mtu huyu aliyejeruhiwa anapelekwa hospitalini baada ya shambulio la bomu Machi 3, 2022. AP - Evgeniy Maloletka
Matangazo ya kibiashara

Pointi kuu:

► Siku moja baada ya jaribio lisilofanikiwa la kuwahamisha raia kutoka Mariupol, mji huu wa bandari uliozingirwa na majeshi ya Urusi, kwa sababu ya kuendelea kwa mashambulizi ya mabomu, mamlaka imetangaza zoei jipya la kuwahamisha raia Jumapili hii saa sita mchana. Kutekwa kwa mji huu webye watu 450,000, uliyoko kwenye Bahari ya Azov,kungewezesha makutano kati ya vikosi vya Urusi vinavyokuja kutoka Crimea iliyounganishwa, ambayo tayari imechukua bandari muhimu za Berdiansk na Kherson, na vikosi vilivyotangaza kujitenga na vikosi vya rusi katika jimbo la Donbass.

► Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema Jumapili kwamba vikosi vya Urusi vinajiandaa kufanya mashambulizi ya anga katika mji wa Odessa, ulioko kusini mwa nchi hiyo.

► Rais wa Urusi Vladimir Putin aapa kuendelea vita: Vikwazo vya Magharibi "ni sawa na tangazo la vita, alisema Jumamosi, kulingana na shirika la habri la Reuters, lakini asante Mungu, bado hatujafika huko."

► Kampuni mbili kubwa za kadi za benki duniani kote Visa na Mastercard walitangaza Jumamosi Machi 5 kwamba wamesitisha shughuli zao nchini Urusi. Kadi za benki za Visa na Mastercard za Kirusi hazitakuwa halali tena nje ya nchi, na kadi zilizotolewa nje ya nchi hazitafanya kazi tena nchini Urusi.

► Kulingana na Rais wa Urusi Vladimir Putin, vikwazo vya Magharibi "ni sawa na tangazo la vita, alisema Jumamosi, kulingana na shirika la habari la Reuters, lakini tunamshukuru Mungu kuwa bado hatujafikia hilo". Kufikia sasa, msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alikuwa ametishia kulipiza kisasi dhidi ya vikwazo hivyo, bila kutoa maelezo zaidi.

► Vyombo vya habari vingi vya Ulaya, ikiwa ni pamoja na BBC, shirika la habari la Marekani Bloomberg na shirika la Uhispania la Efe wamesimamisha kazi ya wanahabari wao wote nchini Urusi, hasa ili kuhakikisha "usalama" wao, baada ya kupitishwa kwa sheria inayotoa adhabu ya kifungo kwa jela kwa utangazaji wa "habari za uwongo kuhusu jeshi".

► Duru mpya ya mazungumzo ya Urusi na Ukraine itafanyika Jumatatu Machi 7, kulingana na mkuu wa ujumbe wa Ukraine.

Naftali Bennett ataka kuendelea na juhudi za ubatanishi

"Hata kama kuna nafasi ndogo ya kufanikiwa, mradi tu kuna uwazi na tunaweza kupata pande zote mbili na uwezo (wa kuchukua hatua), naona ni jukumu la kimaadili kujaribu kila kitu," almesema Waziri Mkuu wa Israeli, wakati wa mkutano wa serikali yake mjini Jerusalem, saa chache baada ya mkutano wake mjini Moscow na Rais Vladimir Putin. "Kama kuna matumaini, lazima tufanye juhudi na bado kunaweza kuwa na wakati wa kuchukua hatua," ameongeza Naftali Bennett.

WHO inashutumu mashambulizi kwenye vituo vya afya

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, WHO, takriban mashambulizi sita kwenye vituo vya afya yamefanyika tangu kuanza kwa vita nchini Ukraine, na kusababisha vifo vya takriban watu sita. Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, anakumbusha kwamba "mashambulizi dhidi ya taasisi za afya yanajumuisha ukiukaji wa sheria za kimataifa za kibinadamu".

Urusi inajiandaa kufanya mashambulizi dhidi ya Odessa, kulingana na Volodymyr Zelensky

"Itakuwa uhalifu wa kijeshi. Itakuwa uhalifu wa kihistoria,” Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema kwenye video kama onyo. Kulingana na Rais Zelensky, askari wa Urusi wanajiandaa kufanya mashambulizi ya anga katika mji wa Odessa, bandari kuu ya Ukraine, iliyoko kwenye mwambao wa Bahari Nyeusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.