Pata taarifa kuu

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kujadili mzozo wa Ukraine

Nchi wanachama 193 wa Umoja wa Mataifa wanakutana katika kikao cha dharura kilichoitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumapili kujadili uvamisi wa Urusi dhidi ya Ukraine. Hatua hii ni ya nadra ambayo iliombwa mara ya mwisho miaka arobaini iliyopita, anakumbusha mwandishi wetu huko New York, Carrie Nooten.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kukutana kwenye makao makuu ya baraza hilo huko New York, kujadili uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kukutana kwenye makao makuu ya baraza hilo huko New York, kujadili uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine. REUTERS/Carlo Allegri
Matangazo ya kibiashara

Azimio la kutaka kusitishwa kwa mapigano nchini Ukraine linatarajiwa kupitishwa wiki hii. Kwa hakika azimio hili halitakuwa na thamani ya kisheria, ni ishara tu, lakini mazungumzo kuhusianana azimio hilo na matokeo ya kura itafanya iwezekanavyo kuona ni nchi gani zinazounga mkono Urusi kwenye katika nyanja ya kimataifa.

Hayo yanajiri wakati, huko Geneva, kikao cha Baraza la Haki za Kibinadamu pia kinaanza Jumatatu hii, na shambulio la Urusi dhidi ya Ukraine bila shaka litakuwa kwenye ajenda ya mazungumzo. Kisha, alasiri ya leo, mkutano mwingine wa Baraza la Usalama, kwa ombi la Paris utafanyika. Lengo ni kupitisha azimio la kuhakikisha ufikiaji usiozuiliwa wa kibinadamu ili kukidhi mahitaji ya watu waliosalia nchini Ukraine.

Ufaransa inataka hili litatuliwe haraka, lakini Urusi inaweza kulipinga. Hatimaye, Kiev ilisawilisha malalamiko yake kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Haki huko The Hague jana Jumapili: Ukraine inaishutumu Urusi kwa kupanga vitendo vya mauaji ya kimbari na kuomba Mahakama kuingilia kati ili kuzuia madhara yasiyoweza kurekebishwa kwa haki za raia wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.