Pata taarifa kuu

Ukraine: 'Dunia haiwezi kuishi bila mafuta au gesi ya Urusi' licha ya wito wa kuwekewa vikwazo

Wakati mzozo wa Ukraine umeanza kuleta athari kwa bei ya mafuta, Waziriwa Mambo ya Nje wa Ukraine Jumamosi Februari 26 ametoa wito kwa nchi za Magharibi "kuweka vikwazo kwa mafuta ya Urusi". Lakini hatua kama hiyo "haiwezi kutekelezwa", kwa sababu Urusi ni nchi ya pili kwa kuuza mafuta ghafi nje ya nchi, ikitoa 11.5% ya usambazaji wa mafuta, kulingana na Pierre Terzian, mtaalam wa maswala ya mafuta.

Urusi ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa uzalishaji wa mafuta na gesi duniani. Hapa, nembo ya kampuni ya Gazprom ya Urusi kwenye moja ya vituo vyake vya gesi huko Moscow, Aprili 16, 2021.
Urusi ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa uzalishaji wa mafuta na gesi duniani. Hapa, nembo ya kampuni ya Gazprom ya Urusi kwenye moja ya vituo vyake vya gesi huko Moscow, Aprili 16, 2021. AFP - KIRILL KUDRYAVTSEV
Matangazo ya kibiashara

► Fuatilia moja kwa moja mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine

"Itenge Urusi, weka vikwazo vya mafuta, haribu uchumi wake": huu ndio wito ambao Waziri wa Mambo ya nje wa Ukraine ametoa kwa viongozi duniani kote.

Lakini vikwazo hivyo haviwezi kufikirika, kulingana na Pierre Terzian, mkurugenzi wa jarida la kila wiki la Petrostratégie, mtaalamu wa masuala ya mafuta, kwa sababu Urusi ni nchi ya tatu kwa uzalishaji mkubwa duniani.

Ukweli wa ukatili ni huu: ulimwengu hauwezi kuishi bila mafuta kutoka Urusi au gesi. Urusi inauza nje zaidi ya mapipa milioni nane kwa siku ya mafuta yasiyosafishwa na bidhaa iliyosafishwa. Hakuna njia ya kubatilisha kiasi hiki. Ni vigumu, kwa kuhamasisha Saudi Arabia kwa 100% na Umoja wa Falme za Kiarabu kwa 100%, kuweza kujaza kati ya mapipa milioni mbili au tatu kwa siku. Lakini nchi nyingine, hazitaweza kupata. Kwa hivyo, kwa bahati mbaya, tishio hili haliwezi kutekelezwa. Madhumuni ya vikwazo hivyo ni kuumiza uchumi wa Urusi na kuilazimisha Moscow kutafuta suluhu. Ikiwa kunaamuriwa vikwazo kwa mafuta au gesi kutoka Urusi, sio Urusi ambayo itateseka, lakini dunia nzima.

Hata bila vikwazo, vita tayari vimekuwa na athari kwa bei ya mafuta, kwani Moscow hutoa 11.5% ya usambazaji wa dunia na ni muuzaji mkubwa wa pili duniani: bei ya mafuta na gesi inaongezeka. Mafuta yalipanda zaidi ya dola 100 kwa pipa, na kufikia dola 105 siku ya Alhamisi (Februari 24), bei ambayo ni ya juu zaidi katika kipindi cha miaka minane.

Huku takriban mapipa milioni 2.3 ya mafuta ghafi ya Urusi yakiondoka kwenda Ulaya kila siku, soko litaendelea kuwa tete mradi tu mzozo utaendelea, kulingana na Pierre Terzian.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.