Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Joe Biden kukutana na washirika kuratibu majibu

Siku ya tano ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, mazungumzo "bila masharti" yamekubaliwa na Ukraine. Muzungumzo hayo yatafanyika kwenye mpaka na Belarus, karibu na mji wa Chernobyl. Mji mkuu wa Kiev unaonekana kujizatiti kwa mashambulizi na kupunguza kasi ya majeshi ya Urusi kwa minajili ya kuudhibiti mji huo. Mkutano Mkuu usio wa kawaida wa Umoja wa Mataifa unatarajia kufanyika leo Jumatatu tarehe 28 Februari.

Rais wa Marekani Joe Biden katika Ikulu ya White House huko Washington, Marekani, Februari 25, 2022.
Rais wa Marekani Joe Biden katika Ikulu ya White House huko Washington, Marekani, Februari 25, 2022. © REUTERS / Leah Millis
Matangazo ya kibiashara

Pointi kuu:

► Baada ya mapigano makali, hasa huko Kharkiv, mji wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine kaskazini-mashariki mwa nchi, mazungumzo kati ya Urusi na Ukraine yanatarajiwa kufanyika kwenye mpaka wa Belarus.

► Vladimir Putin ametangaza kwamba  meviweka kwenye tahadhari ''maalumu'', vikosi vyake vya nyuklia akilalamika kuhusu "taarifa za uchokozi" kuhusu Ukraine zinazotolewa na viongozi wa Nato. Tangazo hilo limezua taharuki duniani kote.

► Ruble (pesa ya Urusi) ilishuka kwa karibu 30% dhidi ya dola Jumatatu baada ya mataifa yenye nguvu ya kimataifa kuweka vikwazo vipya vya kiuchumi dhidi ya Moscow.

► Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana limechukua hatua ya nadra ya kuitisha mkutano wa dharura wa wanachama wote 193 wa Baraza Kuu la Umoja huo kujadili kuhusu azimio la kulaani uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

► Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen alionyesha uungaji mkono usio na shaka kwa uanachama wa Ukraine kwa Umoja wa Ulaya, akiita nchi hiyo "mmoja wetu". EU imeahidi kuipa Ukraine ndege za kivita kwa Ukraine.

► Ripoti ya hivi punde ya Jumapili Februari 27 inaripoti kuwa raia 352 waliuawa, wakiwemo watoto 14, na raia 1,684 kujeruhiwa, wakiwemo watoto 116, kulingana na Waziri wa Afya wa Ukraine. Wakimbizi wapatao 368,000 tayari wamekimbia mapigano, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.