Pata taarifa kuu

NATO yaimarisha mfumo wake wa ulinzi katika nchi zinazopakana na Ukraine

NATO imeanza kupeleka wanajeshi  kutoka kikosi chake cha Kujibu ili kuimarisha zaidi mfumo wake wa ulinzi na kuweza kukabiliana haraka na hali yoyote kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

Vifaru vikisafirishwa kwenye majukwaa ya lori za kijeshi kama sehemu ya kuwasili kwa wanajeshi na vifaa vya ziada vya jeshi la Uingereza katika kambi ya Mapigano ya NATO huko Tapa, Estonia, Ijumaa Februari 25, 2022.
Vifaru vikisafirishwa kwenye majukwaa ya lori za kijeshi kama sehemu ya kuwasili kwa wanajeshi na vifaa vya ziada vya jeshi la Uingereza katika kambi ya Mapigano ya NATO huko Tapa, Estonia, Ijumaa Februari 25, 2022. AP - Sergei Stepanov
Matangazo ya kibiashara

"Vikosi vya Ukraine vinapigana kwa ujasiri na vinaweza kuleta uharibifu kwa vikosi vya Urusi vilivyovivamia," Jens Stoltenberg, Katibu Mkuu wa NATO, alisema baada ya mkutano wa kilele wa shirika hilo siku ya Ijumaa. "Tunapeleka Kikosi cha kujibu kwa mara ya kwanza kama sehemu ya ulinzi wa pamoja ili kuepusha uvamizi wowote katika eneo la muungano," alisema.

Kikosi cha Kujibu cha Pamoja cha Ulinzi kina wanajeshi 40,000 na kiongozi wake ni Kikosi Kazi cha Pamoja chenye umahiri mkubwa (VJTF) chenye wapiganaji 8,000 wanaoongozwa na Ufaransa kwa sasa.

Shambulio la mtandao dhidi ya moja ya nchi 30 za NATO linaweza kuamsha ulinzi wa pamoja wa washirika, alionya Jens Stoltenberg. "Urusi imezindua uvamizi wa jumla dhidi ya Ukraine kwa lengo lililowekwa la kupindua serikali kwa kuandamana hadi Kiev", alisisitiza, kabla ya kuongeza: "Lakini malengo ya Kremlin sio Ukraine pekee". "Putin amedai kuondolewa kwa vikosi vya Muungano kutoka kwa maeneo ya nchi zote ambazo zimejiunga tangu 1997," alikumbusha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.