Pata taarifa kuu

Historia na kumbukumbu ya Holocaust Ulaya, miaka 80 baadaye

Kuanzia 1941 hadi 1945, karibu Wayahudi milioni sita waliuawa na Wanazi, ambao hawakuacha hadi kushindwa kwao kukamilika. Holocaust ni neno linalotumika zaidi kuelezea mauwaji ya maangamizi yaliyofanywa na Manazi dhidi ya Wayahudi.

Jumba la makumbusho ya Holocaust
Jumba la makumbusho ya Holocaust © Olivier Favier
Matangazo ya kibiashara

Kila mwaka mwezi Januari, maafisa wa Ujerumani hukumbuka mauaji ya mamilioni ya Wayahudi na makundi mengine ya watu yaliyofanywa na utawala wa Wanazi.

Kambi ya mateso ya wayahudi ya Auschwitz iliyoko kusini mwa Poland ambako mamilioni ya wayahudi waliouwawa enzi za utawala wa kinazi nchini Ujerumani, kawaida kila mwaka zaidi ya watu milioni 2 huitembelea wakitokea kila pembe ya dunia.

Kambi hiyo imetembelewa na zaidi ya watu milioni 49 tangu ilipofunguliwa kwa ajili ya wageni mnamo mwaka 1947.

Pamoja na kambi kuu tatu za mateso za wanazi,zilikuweko pia kambi nyingine  pembeni  za mateso zikiwa na mashine za kuendesha mauaji ya watu.Makumbusho iliyoko katika kambi kuu ya mateso ya Auschwitz peke yake na makumbusho ya kumbukumbu ya waliouwawa ya Birkenau hivi sasa ina ukubwa unaochukua hekari 191.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.