Pata taarifa kuu
UFARANSA-UCHAGUZI

Macron kutangaza nia ya kugombea urais

Wakati vyama mbalimbali vya siasa nchini Ufaransa vikijiandaa kwa uchaguzi unaopangwa kufanyika mwaka ujao, rais wa nchi hiyo Emmanuel Macron hajasema iwapo atawania muhula wa pili katika uchaguzi huo, lakini wachambuzi wa mambo wanasema nia yake iko wazi na kwamba amekuwa akifanya kampeni isiyo rasmi.

Rais Emmanuel Macron amekuwa katika hatihati za kujiandaa kwa uchaguzi wa urais wa mwakani, kulingana na wachambuzi.
Rais Emmanuel Macron amekuwa katika hatihati za kujiandaa kwa uchaguzi wa urais wa mwakani, kulingana na wachambuzi. Ludovic MARIN AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika kile kinachoelezwa na wachambuzi wa siasa nchini Ufaransa ni kuwa rais Emmanuel Macron amekuwa katika hatihati za kujiandaa kwa uchaguzi wa urais wa mwakani, lakini pia katika upande mwengine amekuwa katika kuandaa namna ambavyo Ufaransa itakavyopokea kijiti kuuongoza Umoja wa Ulaya, EU.

Macron mwenye umri wa miaka 43 anatazamiwa kushiriki mahojiano maalum kupitia televisheni moja jijini Paris, Jumatano jioni ambapo atazungumza kuhusu siasa za ndani ya nchi yake wakati huu akikabiliwa na shutuma kuwa amekuwa akifanya kampeni baada ya mpinzani wake wa muda mrefu Valerie Pecresse pia kuweka wazi nia yake ya kuwania urais.

Wapinzani wengine maarufu ni pamoja na Marine Lepen, Éric Justin Léon Zemmour mwanasiasa wa Ufaransa wa mrengo wa kulia, na mwandishi wa habari za kisiasa, huku wengine wakiendelea kutangaza nia, miongoni mwao Meya wa Jiji kuu la Paris, Anne Hidalgo.

Uchaguzi wa mwaka ujao unaonekana si kipau mbele cha rais Macron ambaye tofauti na watangulizi wake Nicolas Sarkozy na François Hollande ambao hawakufanikiwa kuingia katika muhula wa pili wakiwa madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.