Pata taarifa kuu
UFARANSA-UCHAGUZI

Valérie Pécresse kupeperusha bendera ya chama cha LR katika uchaguzi wa urais

Ni uteuzi wa kihistoria. Kwa mara ya kwanza katika historia yake, chama cha Les Républicains (zamani kikiitwa UMP) kimeamua kuteua mwanamke kupeperusha bendera yake katika uchaguzi wa urais uliopanwa kufanyika mwaka 2022 nchini Ufaransa.

Valérie Pécresse, ni mwanamke wa kwanza kupeperusha bendera ya  chama cha Les Républicains katika uchaguzi wa urais.
Valérie Pécresse, ni mwanamke wa kwanza kupeperusha bendera ya chama cha Les Républicains katika uchaguzi wa urais. © valeriepecresse.fr
Matangazo ya kibiashara

Valérie Pécresse aliteuliwa Jumamosi, Desemba 4, mgombea wa chama cha Les Républicains (LR) katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika mwaka 2022, baada ya kumshinda Eric Ciotti katika duru ya pili ya kongamano iliyoandaliwa mtandaoni na wanachama, alitangaza rais wa chama Christian Jacob.

Rais wa Ile-de-France, anayependwa zaidi kwa msimamo wake wa kiliberali na thabiti, alishinda 60.95% ya kura dhidi ya 39.05% alizopata mbunge wa mrengo wa kulia kutoka Alpes-Maritimes Eric Ciotti.

Valérie Pécresse, ni mwanamke wa kwanza kupeperusha bendera ya  chama cha Les Républicains katika uchaguzi wa rais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.