Pata taarifa kuu

Nchi za umoja wau laya zatakiwa kurejesha hatua dhidi ya Covid-19

Tume ya Umoja wa Ulaya inayohusika na masuala ya afya, inazitaka nchi wanachama, kuanza kurejesha haraka masharti ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona.

Mkurugenzi wa kituo cha cha kuzuiia magonjwa katika bara hilo Andrea Ammon amependekeza mataifa ya Ulaya kuwahimiza watu kuanza kupata chanjo nyingine hasa walio na umri wa miaka 40 na kuendelea ili kuimarisha kinga ya miili yao dhidi ya maambukizi ya Covid-19.
Mkurugenzi wa kituo cha cha kuzuiia magonjwa katika bara hilo Andrea Ammon amependekeza mataifa ya Ulaya kuwahimiza watu kuanza kupata chanjo nyingine hasa walio na umri wa miaka 40 na kuendelea ili kuimarisha kinga ya miili yao dhidi ya maambukizi ya Covid-19. Alberto PIZZOLI AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Mkurugenzi wa kituo cha cha kuzuiia magonjwa katika bara hilo Andrea Ammon amesema hatua hiyo ni muhimu ili kuzuia ongezeko kubwa la maambukizi katika mataifa mbalimbali kati ya mwezi Desemba na Januari.

Aidha, amependekeza mataifa ya Ulaya kuwahimiza watu kuanza kupata chanjo nyingine hasa walio na umri wa miaka 40 na kuendelea ili kuimarisha kinga ya miili yao dhidi ya maambukizi ya Covid-19.

Wito huu unakuja, baada ya Austria wiki hii kuanza kutekeleza masharti ya watu kutotembea kufuatia maambukizi ya virusi hivyo katika siku za hivi karibuni.

Mpaka sasa barani Ulaya, asilimia 67.7 ya watu nchini humo wamepata chanjo kamili, wakati huu ikihofiwa kuwa kirusi aina ya Delta huenda kikasambaa tena.

Shirika la Afya Duniani linaonya kuwa iwapo hatua hazitachukuliwa huenda watu 700,000 wakapoteza maisha barani Ulaya na Asia ya Kati kufikia mwezi Machi mwaka 2022.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.