Pata taarifa kuu
ULAYA

WHO yatiwa wasiwasi na kuendelea kwa janga la COVID-19 Ulaya

Shirika la Afya Duniani, WHO, katika kanda ya Ulaya, linaonya kuwa vifo 236,000 vinavyotokana na COVID-19 vinatarajiwa kuripotiwa ndani ya miezi mtatu ijayo ikiwa hakuna hatua zitakazo chukuliwa kudhibiti hali hiyo.

Chanjo ikitolewa katika kituo cha afya, huko Niš, Serbia, mnamo Machi 3, 2021. Nchi ambazo zinazopatikana mashariki mwa bara la Ulaya zashtumu ucheleweshaji wa chanjo kutoka nchi tajiri za Ulaya Magharibi.
Chanjo ikitolewa katika kituo cha afya, huko Niš, Serbia, mnamo Machi 3, 2021. Nchi ambazo zinazopatikana mashariki mwa bara la Ulaya zashtumu ucheleweshaji wa chanjo kutoka nchi tajiri za Ulaya Magharibi. REUTERS - MARKO DJURICA
Matangazo ya kibiashara

Ulaya tayari imeathirika zaidi na janga la COVID-19, baada ya kurekodi vifo milioni 1.3, huku visa vipya vya maambukizi vikiongezeka kwa zaidi ya 10% katika kipindi cha siku 14 zilizopita katika nchi nyingi barani Ulaya, kulingana na WHO katika kanda ya Ulaya ambayo inajumuisha Asia ya Kati.

Wiki iliyopita, idadi ya vifo kutokana na Corona iliongezeka kwa 11%. Kati ya nchi wanachama wa eneo hilo, 33 zilirekodi ongezeko la zaidi ya 10% kwa kipindi zaidi ya wiki mbili, WHO imesema. Nchi za Balkan, Asia ya Kati na Caucasus zimeathiriwa zaidi.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO barani Ulaya Hans Kluge amesema hali ya utoaji chanjo kwa baadhi ya mataifa bado iko chini na maambukizi aina ya Delta yameonekana kuongezeka, lakini pia mataifa mbalimbali yamelegeza masharti ya kuzuia maambukizi hayo kusambaa.

Hata hivyo rais wa tume ya Ulaya Ursula von der Leyen amesema Umoja huo umefanikiwa kuwapa chanjo kamili asilimia 70 ya watu ambao ni zaidi ya watu milioni 250 ndani ya Umoja huo.

Katika taarifa fupi kwa njia ya video, von der Leyen amesema ni mafanikio makubwa na ya kupigiwa mfano ya Umoja huo kutimiza lengo walilojiwekea la kutoa chanjo ya umma dhidi ya Covid-19.

von der Leyen amewataka watu kuchukua tahadhari kwani janga la ugonjwa wa Covid-19 bado lingalipo, na kutoa wito kwa watu kuchomwa chanjo ili kuepuka wimbi jipya la maambukizo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.