Pata taarifa kuu
EU-AFYA

Covid-19: Umoja wa Ulaya kupunguza idadi ya nchi zinazoonekana kuwa salama

Idadi ya nchi ambazo wakaazi wao wanaweza kuingia katika nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) bila vizuizi vya kiafya itapunguzwa tena kuanzia Jumatatu, Agosti 30. Ramani mpya ya magonjwa duniani iliyopitishwa Ijumaa itapunguza tena idadi ya nchi zinazochukuliwa kuwa salama na Umoja wa Ulaya.

Katika uwanja wa ndege wa Roissy-Charles-de-Gaulle. Ikiwa ni pamoja na Marekani, jumla ya nchi na maeneo sita yamechukuliwa tena masharti ya kuingia Umoja wa Ulaya.
Katika uwanja wa ndege wa Roissy-Charles-de-Gaulle. Ikiwa ni pamoja na Marekani, jumla ya nchi na maeneo sita yamechukuliwa tena masharti ya kuingia Umoja wa Ulaya. AP - Francois Mori
Matangazo ya kibiashara

Nchi hizi ishirini na saba, wanachama wa Umoja wa Ulaya, wameacha mipaka yao wazi kwa washirika wao katika eneo la Uchumi lkutoka Ulaya (Uswizi, Liechtenstein, Norway na Iceland) na pia kwa majimbo manne ambayo hayana bahari huko Ulaya. Watu kutoka nchi zingine zote duniani hupimwa mara kwa mara kwa msingi wa kiwango chao cha maambukizi virusi vya Covid-19 na chanjo yao. Na Marekani ni moja wapo ya nchi ambazo hazina kinga ya kutosha kuingia Ulaya.

Ikiwa ni pamoja na Marekani, jumla ya nchi na maeneo sita yamejikuta yakiwekewa tena masharti na Umoja wa Ulaya ya kuingia katika nchi wanachama wa umoja huo. Uamuzi huo mpya ulichukuliwa Ijumaa na mabalozi wa kudumu kutoka nchi ishirini na saba, wanachama wa Umoja wa Ulaya, huko Brussels: pia zimeondoa kwenye orodha yao nchi na maeneo matatu ya Balkan (Montenegro, Kosovo na North Macedonia)pamoja na Israeli na Lebanon.

Safari muhimu tu

Hazizingatiwi tena kuwa salama kutokana na hali ya janga la Corona na kwa hivyo wakaazi wao hawaruhusiwi tena kuingia Umoja wa Ulaya na eneo la Schengen isipokuwa kwa safari muhimu.

Hakuna nchi ya Kiafrika inayoonekana kuwa salama tangu kujiondoa kwa Rwanda katikati ya mwezi wa Julai.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.