Pata taarifa kuu
EU

Coronavirus: EU kutathmini upya orodha ya maeneo salama

Umoja wa Ulaya itapitia wiki ijayo orodha ya maeneo ambayo safari isiyo ya lazima inaruhusiwa licha ya vizuizi vilivyowekwa kupambana na mlipuko wa Corona na unaweza kutafakari tena sheria ya Marekani, mwakilishi wa umoja huo amesema Ijumaa wiki hii

Umoja wa Ulaya unatathmini upya mara kwa mara orodha yake kufuata maendeleo ya janga hilo.
Umoja wa Ulaya unatathmini upya mara kwa mara orodha yake kufuata maendeleo ya janga hilo. AFP - TOLGA AKMEN
Matangazo ya kibiashara

Orodha hii kwa sasa inakusanya karibu nchi kumi, ikiwa ni pamoja na Marekani, Japani na Australia, ambazo zinahesabiwa kuwa sehemu salama kwa suala la janga hilo.

Mkutano wa wiki ijayo "unaweza" kutathmini hali nchini Marekani, afisa huyo wa Umoja wa Ulaya ameliambia shirika la habari la REUTERS bila kuongeza maelezo zaidi.

Umoja wa Ulaya unatathmini upya mara kwa mara orodha yake kufuata maendeleo ya janga hilo.

Umoja wa Ulaya umeomba Washington mara kadhaa kuruhusu kuingia kwa raia wa Ulaya katika ardhi yake tangu Marekani iongezwe kwenye "orodha nyeupe" (nchi zilizo salama) mwezi Juni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.