Pata taarifa kuu
WHO-AFYA

WHO yaataka kutanguliza chanjo katika nchi masikini kuliko ile ya watoto

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani Tedros Adhanom ametoa wito kwa nchi kuachana na mpango wa kutoa chanjo kwa watoto na vijana dhidi ya janga la COVID-19 na kutoa dozi ambazo zimetolewa kwa mfumo wa Covax ili kuzisambaza tena kwa nchi ambazo zinazihitaji.

Janga la Covid-19 laendelea kusababisha vifo vingi na maambukizi makubwa duniani.
Janga la Covid-19 laendelea kusababisha vifo vingi na maambukizi makubwa duniani. GABRIEL BOUYS AFP
Matangazo ya kibiashara

Tedros Adhanom Ghebreyesus amebaini kuwa jinsi mambo yanavyokwenda, mwaka wa pili wa janga hilo "utakuwa mbaya zaidi" kuliko ule wa kwanza. Ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari.

"Ninaelewa ni kwanini baadhi ya nchi zinataka kutoa chanjo kwa watoto wao na vijana, lakini ninawaomba fikiria kuachana na mpango huo na badala yake kutoa chanjo katika mpango wa Covax", mfumo wa kimataifa uliowekwa kuhakikisha upatikanaji wa chanjo sawa, amesema mkurugenzi mkuu ya WHO.

Kwa miezi kadhaa, amelaani mwenendo wa nchi kadhaa kutia mbele utaifa katika utoaji chanjo, kwa sababu ya uhaba wa dozi zilizopo, hali ambayo inanyima nchi nyingi kuweza kulinda, ikiwa ni pamoja na watu walio katika mazingira magumu zaidi na wahudumu wa afya, wakati moja wa Ulaya au Marekani ikiahidi kuchanja idadi kubwa yaraia wake kwa msimu wa joto.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.