Pata taarifa kuu

Covid-19: Nchi kumi za Umoja wa Ulaya zakabiliwa na hali 'ya wasiwasi'

Hali ya janga la Covid-19 inaendelea kuzorota katika nchi za Umoja wa Ulaya na inachukuliwa kuwa "ya wasiwasi sana" katika nchi kumi na "ya wasiwasi" katika zingine kumi, shirika la Ulaya linalojihusisha na magonjwa limesema Ijumaa.

Watu wamepanga foleni ili kuchanjwa huko Zagreb Novemba 4, 2021. Kroatia ni miongoni mwa nchi 10 za Umoja wa Ulaya ambapo hali ya afya inachukuliwa kuwa "ya wasiwasi sana"
Watu wamepanga foleni ili kuchanjwa huko Zagreb Novemba 4, 2021. Kroatia ni miongoni mwa nchi 10 za Umoja wa Ulaya ambapo hali ya afya inachukuliwa kuwa "ya wasiwasi sana" AP - Darko Bandic
Matangazo ya kibiashara

Maambukizi ya virusi vya Corona yanaongezeka tena barani Ulaya, hadi kulazilazimu nchi kadhaa kupanga kurejesha vizuizi vya kukabiliana na maambukizi.

Katika tathmini yake ya hivi punde ya hatari, Kituo cha Ulaya cha Kudhibiti Magonjwa (ECDC) kinabaini

 kwamba hali ya magonjwa katika nchi za Umoja wa inakwenda sambamba na ongezeko la haraka na kubwa la kesi, na kiwango cha chini cha vifo kinaongezeka polepole. "Kesi za maambukizi, kesi za waginjwa kulazwa hospitalini na idadi ya vifo vyote vinatarajiwa kuongezeka katika muda wa wiki mbili zijazo," limesema shirika hilo la Ulaya lenye makao yake mjini Stockholm.

Hali hiyo inachukuliwa kuwa "ya wasiwasi sana" katika nchi kumi: Ubelgiji, Poland, Uholanzi, Bulgaria, Kroatia, Jamhuri ya Czech, Estonia, Ugiriki, Hungary na Slovenia. Nchi zilizo katika kiwango cha "wasiwasi" ni pamoja na Ujerumani, Austria, Denmark, Finland, Ireland, Latvia, Lithuania, Luxembourg, Romania na Slovakia. Nchi tatu ambazo ziko katika kiwango cha "wasiwasi wa wastani" (Ufaransa, Ureno, Cyprus) huku nchi nne zikiwa katika kiwango cha wasiwasi mdogo (Italia, Uhispania, Uswidi na Malta). Kwa nchi nyingine tatu zisizo wanachama wa EU zinazofuatiliwa na kituo hiki cha Ulaya cha kudhibiti magonjwa (Norway, Iceland na Liechtenstein), hali hiyo inachukuliwa kuwa "ya wasiwasi".

Njia inayotumiwa na kituo cha ECDC kwa aina za wasiwasi inachanganya maadili kamili (idadi ya kesi za maambukizi, kulazwa hospitalini na vifo) lakini pia mabadiliko yao ya hivi karibuni. Kulingana na makadirio yake ya hivi karibuni, idadi ya kesi na vifo inatarajiwa kuongezeka kwa karibu 50% katika wiki mbili zijazo, na kufikia kiwango cha kila wiki cha kesi mpya 300 na vifo 2.7 kwa kila watu 100,000.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.