Pata taarifa kuu
UJERUMANI-SIASA

Uchaguzi wa wabunge Ujerumani: SPD na CDU / CSU wakaribiana kwa kura

Jioni ya uchaguzi wa wabunge nchini Ujerumani, makadirio ya matokeo ya awali yanaonesha mchuano mkali kati ya vyama vya CDU/CSU na SPD. 

Katika makao makuu ya chama cha CDU huko Berlin, ambapo makadirio ya awali yakitangazwa, Septemba 26, 2021.
Katika makao makuu ya chama cha CDU huko Berlin, ambapo makadirio ya awali yakitangazwa, Septemba 26, 2021. AFP - JOHN MACDOUGALL
Matangazo ya kibiashara

Makadirio yanonesha kuwa vyama hivyo vimepata asilimia 25 kila mmoja, wakati makadirio hayo yamekiweka chama cha watetezi wa mazingira, die Grüne, katika nafasi ya tatu kwa ailimia 15. Takwimu ambazo zinachukuliwa kwa uangalifu, ikizingatiwa umuhimu wa kura kupitia njia ya posta.

Kulingana na makadirio ya awali yaliyotangazwa jioni ya Jumapili hii, muungano wa vyama vya CDU / CSU na chama cha SPD vimepata 25% ya kura, sawa na idadi sawa ya viti katika Bunge. Vyama hivyo vitakuwa na fursa ya kukaa madarakani na kuunda muungano, amebaini mwandishi wetu huko Berlin, Pascal Thibaut.

Kura hizi za awali zimepokelewa kwa furaha katika makao makuu ya chama cha SPD huko Berlin. Katibu mkuu wa chama hicho, Lars Klingbeil, alisema wako tayari kuunda serikali ijayo. “Tuna jukumu la kuunda serikali. Olaf Scholz atakuwa kansela, ”ametangaza.

Chama cha mrengo wa kulia cha AfD kimeshuka kwa alama 1.5 ikilinganishwa na mwaka 2017. Chama cha mrengo wa kushoto Die Linke ni kimepata 5% tu, kura zinazohitajika kwa kuwakilishwa katika bungni (Bundestag).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.