Pata taarifa kuu
UJERUMANI-SIASA

Ujerumani kupiga kura kuwachagua wabunge na Kansela

Wajerumani wanapiga kura, Jumapili hii, Septemba 26, 2021, kuwachagua viongozi wao hususan wabunge na Kansela kabla ya miezi kadhaa ya mazungumzo ya kuunda serikali mpya. Wajerumani wapatao milioni 60.4 ambao wana umri zaidi ya miaka 18 wanaweza kupiga kura.

Angel Merkel wakati wa hotuba kwa kampeni ya uchaguzi wa wabunge Septemba 24 huko Munich.
Angel Merkel wakati wa hotuba kwa kampeni ya uchaguzi wa wabunge Septemba 24 huko Munich. AP - Matthias Schrader
Matangazo ya kibiashara

Wajerumani wataweza kuchagua wabunge katika bunge la muungano huko Bundestag, na kuna viti vipatavyo 598 na mara nyingi zaidi ya hapo.

Kuondoka kwa Kansela Angela Merkel, madarakani tangu 2005, kunafunua ukurasa mpya wa kisiasa. Ni mara ya kwanza tangu mwaka 1949 kansela anayemaliza muda wake hawanii kwenye wadhifa huo. Mwsali yameibuka kuhusu upande gani utapata utashinda uchaguzi huo na kurithi muungano wa kati kati ya wahafidhina kutoka muungano wa vyama vya CDU / CSU na chama cha SPD.

Angela Merkel amejiondoa kwene kinyang'anyiro hicho baada ya kutawala nchi hiyo kwa karibu miaka 16, na ni kiongozi wa pili kukaa madarakani muda mrefu baada ya Helmut Kohl.

Mgombea wa Ukansela wa chama cha SPD Olaf Scholz, 63, ambaye amefanya kazi kwa karibu na Merkel kama waziri wake wa fedha kwa zaidi ya miaka minne iliyopita, ndiye mgombea anayepewa nafasi kubwa ya kushinda. Mpinzani wake mkuu Armin Laschet, 60, kutoka muungano wa vyama vya kihafidhina vya CDU/CSU alikuwa anasuasua wakati wa kampeni lakini amejikongoja na kupunguza pengo katika utafiti wa kura za maoni kwa asilimia kidogo katika siku za hivi karibuni.

Vituo vya kuoigia kura vitafungwa saa 12 jioni, na matokeo ya uchaguzi yataanza kuolewa baada ya kura za awali kuhesabiwa.

Bi Merkel aliahidi kutofanya kampeni siku ya uchaguzi ambayo ni Jumapili, lakini muungano wa CDU-CSU umepoteza kile ambacho walikuwa wanajiamini nacho katika kuongoza katika kura na sasa kiko nyuma ya SPD (Social Democrats) - washirika wapya katika serikali ya muungano .

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.