Pata taarifa kuu
UJERUMANI-UCHAGUZI

Wajerumani wajiandaa kupiga kura siku ya Jumapili

Kampeni za mwisho zinafanyika  kuelekea Uchaguzi Mkuu nchini Ujerumani siku ya Jumapili, utakaomaliza uongozi wa miaka 16 wa Kansela Angela Merkel.

Kansela Angela Merkel akiwa na kiongozi wa chama chake cha CDU   Armin Laschet, wakati wa kampeni za mwisho Septemba 25 2021
Kansela Angela Merkel akiwa na kiongozi wa chama chake cha CDU Armin Laschet, wakati wa kampeni za mwisho Septemba 25 2021 AP - Martin Meissner
Matangazo ya kibiashara

Wapiga kura wapatao Milioni 60 walio na zaidi ya umri wa miaka 18 wanatarajiwa kushiriki kwenye Uchaguzi huo, kuwachagua wabunge 598.

Wachambuzi wa siasa wanasema, utachaguzi huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkali kati ya chama cha Kansela Merkel cha CDU na kile cha mrengo wa Kushoro cha SPD.

Tayari Merkel ameunga mkono kiongozi wa chama chake Armin Laschet kumrithi, anapomaliza muda wake wa uongozi nchini humo.

Katika kampeni ya mwisho siku ya Jumamosi, Kansela Merkel amempigia debe Laschet na kuwataka Wajerumani kumchagua wakati huu kura za maoni zikionesha kuwa yupo nyuma ya mgombea wa   SPD Olaf Scholz.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.