Pata taarifa kuu
UJERUMANI-MAZINIRA

Mahakama ya Ulaya ya Haki: Ujerumani ilivunja sheria za uchafuzi wa mazingira

Ujerumani "imevuka" mara kadhaa mfululizo "viwango vya uchafuzi wa hewa vya Umoja wa Ulaya (EU), Mahakama ya Haki ya Ulaya, ECJ, imesema leo Alhamisi katika uamuzi ambao unaweza kusababisha nchi hiyo inachukuliwa vikwazo vya kifedha ikiwa itashindwa kuboresha ubora wa hewa katika miji mikubwa kadhaa.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ahutubia wanahabari kufuatia mkutano na mawaziri wakuu wa majimbo ya Ujerumani Mashariki katika ofisi yake, huko Berlin, Ujerumani Juni 2, 2021.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ahutubia wanahabari kufuatia mkutano na mawaziri wakuu wa majimbo ya Ujerumani Mashariki katika ofisi yake, huko Berlin, Ujerumani Juni 2, 2021. REUTERS - ANNEGRET HILSE
Matangazo ya kibiashara

"Ujerumani (imekiuka) agizo juu ya ubora wa hewa kwa kuvuka mara kada mfululizo, kuanzia Januari 1, 2010 hadi mwaka 2016, kiwango cha kikomo cha mwaka kilichowekwa kwa Hewa ukaa (dioksidi kabonia) katika maeneo 26 kati ya 89 ", inmeandika mahakama ya juu zaidi ya Umoja wa Ulaya katika uamuzi wake.

Miongoni mwa maeneo yanayohusika ni misitu ya Berlin, Stuttgart, Freiburg na Munich.

Ujerumani pia ilivuka, katika kipindi hicho hicho, kiwango cha kikomo cha saa kilichowekwa kwa Hewa ukaa katika maeneo haya mawili, ambayo ni eneo la mji mkuu wa Stuttgart na lile la Rhine-Main, imesema Mahakama ya Haki ya Ulaya.

ECJ imeamua kwamba serikali ya Ujerumani haikuchukua hatua zinazofaa kuhakikisha kufuata sheria za ubora wa hewa za Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.