Pata taarifa kuu
ULAYA-MAREKANI

Macron na Merkel wataka Marekani kujieleza kuhusu udukuzi dhidi ya nchi zao

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, wamesema wanatarajia Marekani na serikali ya Denmark kufafanua madai kuwa, Washington DC imekuwa ikifuatilia mawasiliano ya viongozi wa siasa wa mataifa kadhaa barani Ulaya kutoka Copenhagen.

Kansela wa Ujerumani Merkel na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.
Kansela wa Ujerumani Merkel na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron. Tobias SCHWARZ / AFP
Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao wawili wa mataifa hayo ya bara Ulaya wamesema kuwa kitendo cha Marekani hakikubaliki, na hakistahili kuwepo kati ya washirika wa karibu, ikizingatiwa kuwa mataifa ya Ulaya na Marekani yana ushirikiano wa karibu.

Rais Macron amesema kwa kipindi kirefu, Marekani na mataifa ya Ulaya yamekuwa yakiamini na hivyo hakuna hata nafasi ya upande mmoja kumshuku mwenzake.

Kansela Merkel naye amesema anakubaliana na kauli ya Macron kuhusu Marekani na Denmark kutoa maelezo kuhusu madai hayo.

Haya yanajiri baada ya Redio ya taifa nchini Denmark na vyombo kadhaa vya Habari barani Ulaya kuripoti kuwa, Shirika la usalama nchini Marekani  liliweka mtambo maalum wa mawasiliano kati ya mwaka 2012 na 2014 unaotumia, mtandao wa Internet, kusikiliza mawasilliano ya wanasiasa kutoka Ujerumani, Sweden, Norway na Ufaransa kwa kusikiliza mawasiliano ya simu lakini pia kusoma barua pepe na ujumbe mfupi wa simu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.