Pata taarifa kuu
WHO-AFYA

WHO yatoa hakikisho juu ya chanjo ya AstraZeneca

Je! Chanjo ya AstraZeneca husababisha athari mbaya? Swali hili limezua sintofahamu barani Ulaya, kwani Ufaransa, Ujerumani, Uhispania na Italia zilitangaza - siku ya Jumatatu - kusitisha kampeni ya kutoa chanjo hiyo na kutumia bidhaa zote kutoka kampuni ya AstraZeneca.

Hakuna sababu, ya kutotumia chanjo AstraZeneca kwa kuwachanja raia kwa madai yasiyo kuwa na msingi, yaonya WHO.
Hakuna sababu, ya kutotumia chanjo AstraZeneca kwa kuwachanja raia kwa madai yasiyo kuwa na msingi, yaonya WHO. Claudio CRUZ AFP
Matangazo ya kibiashara

Shirika la madawa la Umoja wa Ulaya (EMA), ambalo limekutana katika kikao cha dharura, linatarajia kutoa taarifa haraka iwezekanavyo.

Wakati huo huo shirika la Afya duniani (WHO) limetoa hakikisho kwamba chanjo ya AstraZeneca inafanya kazi kwa ufanisi mkubwa.

Hakuna sababu, ya kutotumia chanjo AstraZeneca kwa kuwachanja raia kwa madai yasiyo kuwa na msingi.

Awali shirika la Afya Duniani lilisema mataifa hayapaswi kusitisha matumizi ya chanjo ya Corona ya AstraZeneca kwa kuhofia kusababisha kuganda kwa damu wakati hakuna ukweli wowote juu ya hilo.

Madai ya kuganda kwa damu yafutilia mbali

Mkuu wa kitengo cha Sayansi katika shirika la Afya Duniani, Soumya Swaminathan, anasema anaelewa hofu ya nchi za Ulaya.

Angalau watu milioni 2.6 tayari wamefariki dunia kutokana na COVID. Na kati ya dozi milioni 300 za chanjo ambazo tayari zimeshatolewa kote ulimwenguni, hakujakuwa na vifo vilivyohusishwa moja kwa moja na chanjo yoyote [haijalishi ni ipi]. Kwa hivyo ninaamini kwamba ikiwa tunapaswa kusoma hali hiyo kwa karibu sana, hatutaki watu waendelee kuwa na hofu. Kwa sasa, tunapendekeza kwamba nchi ziendelee kutoa chanjo ya [AstraZeneca]. Lakini tutajua zaidi hivi karibuni.

Bulgaria, Denmark na Norway ni miongoni mwa mataifa ambayo yamesitisha matumizi ya chanjo hiyo.

Siku ya Ijumaa, msemaji wa WHO amesema hakuna uhusiano wowote baina ya chanjo hiyo na hatari ya watu kuganda damu.

Margaret Harris amesema chanjo hiyo ni salama na iendelee kutumika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.