Pata taarifa kuu
Ghana-Corona-COVAX

Ghana yapokea chanjo 600,000 ya COVID-19

Shirika la afya duniani WHO, kupitia kwa mpango wake wa kutoa mgao wa chanjo ya covid 19, COVAX, limewasilisha dozi 600,000 ya chanjo aina ya AstraZeneca, nchini Ghana.

Ghana  kupokea dozi 600,000 ya chanjo ya corona aina ya AstraZeneca/Oxford
Ghana kupokea dozi 600,000 ya chanjo ya corona aina ya AstraZeneca/Oxford © THOMAS KIENZLE AFP
Matangazo ya kibiashara

Mwakilishi wa WHO, nchini Ghana, Francis Kasolo, baada ya kupokea chanjo hiyo, amesema kuwasili kwa chanjo hiyo nchini Ghana ni hatua muhimu katika mchakato wa kumaliza maambukizi nchini humo.

 

Kuwasili kwa chanjo hiyo kumejiri miezi nane baada ya kuzinduliwa kwa mpango wa COVAX, ambao unahakikisha mataifa yanayoendelea duniani yanapokea chanjo ya virusi vya corona.

Ghana sasa inaweka mikakati kuhakikisha raia wake wanaanza kupokea chanjo hiyo kuanzia machi tarehe mbili, wahudumu wa afya wakiwa wa Kwanza kuipokea pamoja na raia walio na umri wa zaidi ya miaka 60.

Bara Afrika hadi wakati huu limesajili visa zaidi ya laki moja vya vifo ambavyo vimetokana na COVID 19.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.