Pata taarifa kuu
GHANA-AFYA-UCHUMI

COVID: Rais wa Ghana adungwa sindano ya kwanza ya chanjo ya COVAX

Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo, 76, ambaye nchi yake ndio ya kwanza duniani kupokea chanjo ya mpango wa Umoja wa Mataifa wa COVAX Jumatano wiki iliyopita, amedungwa sindano ya kwanza ya chanjo dhidi ya ugonjwa huo, kulingana na picha zilizorushwa moja kwa moja na runinga ya taifa ya Ghana.

Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo huko Accra.
Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo huko Accra. AP - Ofoe Amegavie
Matangazo ya kibiashara

"Ni muhimu zoezi hili nilizindue mimi kwa kudungwa sindano, kutoa mfano mzuri kwa raia na kuonyesha kwamba chanjo hii ni salama kwa watu wote, ili kila mtu nchini Ghana ajisikie vizuri kupata chanjo," rqis Nana Akufo-Addo amesema katika hotuba.

Mfumo wa COVAX unakusudia kutoa chanjo dhidi ya COVID-19 kwa 20% ya wakaazi kutoka karibu nchi 200 na majibmbo yanyoshiriki mwaka huu, lakini muhimu zaidi ina utaratibu wa ufadhili ambao unawezesha nchi 92 zenye uchumi wa kiwango cha chini na cha kati kupata chanjo hii yenye thamani. Mfumo huo ulianzishwa ili kujaribu kuzuia nchi tajiri kuchukua viwango vyote vya chanjo ambavyo bado vinatengenezwa kwa idadi ndogo sana ili kukidhi mahitaji ya dunia.

Ghana taifa la kwanza duniani kupokea chanjo ya COVAX

Covax imefikia makubaliano na watengenezaji wa chanjo kwa dozi bilioni mbili mnamo mwaka 2021 na ina uwezo wa 'kununua bilioni nyingine. Ghana Jumatano imekuwa taifa la kwanza ulimwenguni kupokea dozi za chanjo inayofadhiliwa na mpango huo.

Nchi hii inayozungumza Kiingereza Magharibi mwa Afrika imerekodi visa 84,023 vya maambukizi ya virusi vya Corona, pamoja na vifo 607.

Ghana imepanga kutoa chanjo kwa raia wake Milioni 20 kati ya milioni 30 kabla ya mwisho wa mwaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.