Pata taarifa kuu
IRAN

Rohani akaribisha kuondoka mamlakani kwa Donald Trump

Rais wa Iran Hassan Rouhani amekaribisha kuondoka mamlakani kwa rais wa Marekani Donald Trump, ambaye amemtaja kama "gaidi" na "rais wa Marekani aliyekosolewa zaidi katika historia".

Rais wa Iran, Hassan Rouhani.
Rais wa Iran, Hassan Rouhani. Iranian Presidency / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Hatufurahii kuwasili kwa Bw. Biden, lakini tunayo furaha kuona Trump anaondoka mamlakani," Hassan Rouhani amesema katika hotuba ya televisheni.

Hayo yanajiri wakati rais wa Brazil Jair Bolsonaro alimpongeza rais mteule wa Marekani Joe Biden Jumanne, Desemba 15, kwa ushindi wake mwezi Novemba, na kuongeza kuwa "yuko tayari kufanya kazi" na mrithi wa Donald Trump, mfano mzuri wa kiongozi kutoka mrengo wa kulia.

Bolsonaro ndiye kiongozi wa mwisho wa kundi la mataifa 20 yenye nguvu dunian ,G20, kumpongeza Joe Biden, siku hiyo hiyo na wenzao wa Urusi Vladimir Poutine na Andrés Manuel López Obrador wa Mexico.

Jopo la wajumbe maalumu lenye nguvu ya kumchagua rais wa Marekani, maarufu kama Electoral College lilithibitisha Jumatatu wiki hii ushindi wa Joe Biden kwa kura 306 dhidi ya 232 alizopata Donald Trump.

Hakuna mjumbe hata mmoja kutoka jopo hili" aliyempinga rais mteule Joe Biden.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.