Pata taarifa kuu
UJERUMANI-UFARANSA-EU-CORONA-UCHUMI

Macron na Merkel watoa wito kwa EU kujiandaa vyema kwa mgogoro wa kiafya

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na viongozi wa nchi zingine nne za Ulaya wametoa wito kwa Umoja wa Ulaya kutumia hifadhi ya dawa na vifaa vya matibabu na kuhimiza maendeleo ya pamoja ya chanjo na matibabu ili kukabiliana vilivyo na mgogoro mwengine wa kiafya.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel wamependekeza Umoja wa Ulaya kuwa na hifadhi ya kudumu ya miezi mitatu ya dawa na vifaa na kwamba nchi wanachama ziweze kushirikiana kutoa bidhaa muhimu wakati wa mgogoro wa kiafya.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel wamependekeza Umoja wa Ulaya kuwa na hifadhi ya kudumu ya miezi mitatu ya dawa na vifaa na kwamba nchi wanachama ziweze kushirikiana kutoa bidhaa muhimu wakati wa mgogoro wa kiafya. Oliver Matthys/Pool via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Katika barua ya pamoja kwa rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen Jumanne wiki hii, Rais wa Ufaransa, Kansela wa Ujerumani, Waziri mkuu wa Denmark, Waziri mkuu wa Uhispania, Waziri mkuu wa Ubelgiji na Waziri mkuu wa Poland wametoa wito wa kufikiria kuhusu mkakati wa jumla katika ngazi ya Ulaya, ambao ni wenye ufanisi zaidi kuliko majibu maalum ya nchi.

Wamependekeza Umoja wa Ulaya kuwa na hifadhi ya kudumu ya miezi mitatu ya dawa na vifaa na kwamba nchi wanachama ziweze kushirikiana kutoa bidhaa muhimu wakati wa mgogoro wa kiafya.

Taarifa hiyo pia inasisitiza kuhusu haja ya Umoja wa Ulaya kuendeleza uwezo wa utafiti na maendeleo kuhusu chanjo, hasa kwa kufadhili vipimo vya kliniki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.