Pata taarifa kuu
EU-CORONA-AFYA-UCHUMI

Coronavirus: Nchi 27 za Umoja zakutana kwa lengo la kufufua uchumi

Viongozi kutoka nchi 27 za Umoja wa Ulaya wanakutana Jumatano hii Aprili 23 kwa lengo la kufufua uchumi ambao unaendelea kudorora kila kukicha.

Nchi 27, wanachama wa Umoja aw Ulaya, wanatarajia kukutana leo Jumatano kwa lengo la kufufua uchumi uliodorora kutoka na Covid-19.
Nchi 27, wanachama wa Umoja aw Ulaya, wanatarajia kukutana leo Jumatano kwa lengo la kufufua uchumi uliodorora kutoka na Covid-19. REUTERS/Thierry Roge
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu wa Alhamisi Aprili 23 ni mkutano wa nne unaozileta pamoja nchini 27 za Umoja wa Ulaya tangu kuzuka mgogoro wa kiafya.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanatafuta suluhisho ili kuondoa umoja huo katika mdororo wa uchumi uliosababishwa na janga la Covid-19.

"Nina imani kwa makubaliano ya kwanza". Maneno yanayoleta matumaini zaidi kati ya viongozi kutoka nchi 27 ni yale ya Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez. Madrid imependekeza kutolea kwa euro bilioni 1,500, fedha zitakazochukuliwa kama deni la kudumu kusaidia nchi zilizo kwenye matatizo.

Hata hivyo baadhi ya nchi hazikubaliani kuhusu pendekezo la Uholanzi, licha ya kuwa kuna nchi ambazo zinaunga mkono. Ujerumani na Uholanzi hasa, hawaungi mkono hoja hiyo. Ima kuhusu kiwango, pesa hizo ni ndogo mno, kulinganna na mtazamo wa baadhi ya nchi.

Viongozi kutoka nchi 27 za Umoja wa Ulaya wanatarajia kupata suluhisho kwa tofauti zote hizo kwa lengo la kufufua uchumi wa umoja huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.