Pata taarifa kuu
UJERUMANI-MERKEL-SIASA

Angela Merkel: Huu ndio muhula wangu wa mwisho

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, ambaye umaarufu wake umepunguwa tena tangu kuzuka kwa mgogoro wa kiafya na kiuchumi, amesema Alhamisi wiki hii kuwa hana nia ya kubadili uamuzi wake na kwamba muhula wake wa sasa utakuwa wa mwisho.

Merkel aliingia katika siasa na kuwa kama msemaji wa waziri mkuu wa mwisho katika iliyokuwa Ujerumani Mashariki, Lothar de Maiziere, wakati huo akiwa na umri wa miaka 35.
Merkel aliingia katika siasa na kuwa kama msemaji wa waziri mkuu wa mwisho katika iliyokuwa Ujerumani Mashariki, Lothar de Maiziere, wakati huo akiwa na umri wa miaka 35. John MACDOUGALL / AFP / POOL
Matangazo ya kibiashara

Angela Merkel ameongoza serikali ya shirikisho nchini Ujerumani tangu mwaka 2005.

Kufuatia uchaguzi wa mwisho wa wabunge mwezi Septemba 2017, ambao ulionyesha jinsi gani na kambi yake ya Consrvative CDU-CSU iligawanyika na kupteza umaarufu.

Angela Merkel ameahidi kwamba muhula wake wa nne utakuwa wa mwisho na atatoa nafasi kwa watu wengine kuwania nafasi hiyo mwisho wa muhula wake mwaka 2021.

Merkel aliingia katika siasa na kuwa kama msemaji wa waziri mkuu wa mwisho katika iliyokuwa Ujerumani Mashariki, Lothar de Maiziere, wakati huo akiwa na umri wa miaka 35.

Chini ya Kansela Helmut Kohl mwaka 1994 alikuwa waziri wa mazingira na usalama wa nyuklia, wizara muhimu kabisa kwa mtu anayeshikilia shahada ya uzamifu katika fizikia.

Baada ya kushindwa Helmut Kohl katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1998, chama cha CDU kilipata mshtuko mkubwa lakini sio kwa Merkel, ambaye aliitumia nafasi yake barabara na mwaka 2000 akachaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho.

Mwaka 2005 katika uchaguzi mkuu akatokeza kuwa mgombea mkuu wa chama hicho wa Ukansela. Merkel alipata ushindi lakini ilimbidi kuunda serikali ya pamoja na chama cha SPD. Merkel amekuwa kansela kwa miaka 15.

Tangu mwaka 2008 Kansela Angela Merkel amekuwa akiangaliwa kimsingi kama kiongozi mzuri katika kukabiliana na migogoro. Katika suala la Ugiriki, alisaidia kuikowa sarafu ya euro.

Haijapata kutokea katika historia ya Ujerumani baada ya mwaka 1945 kutokea mwanasiasa aliyewekewa matumani kidogo kama ilivyotokea kwa binti huyo wa mchungaji kutoka Mashariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.