Pata taarifa kuu
ULAYA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Ulaya yajiandaa kulegeza hatua zilizowekwa kudhibiti Corona na kuinua uchumi

Nchi nyingi, hasa barani Ulaya, zinatathmini uwezekano wa kulegeza masharti yaliyowekwa kudhibiti ugonjwa wa Covid-19 ili kutoa nafasi ya kuinua uchumi uliyodorora kutokana na mgogoro wa afya uliosababishwa na ugonjwa wa Covid-19.

Watu milioni 3.1 duniani wameambukizwa virusi vya Corona, tangu ulipozuka huko Wuhan, katikati mwa China.
Watu milioni 3.1 duniani wameambukizwa virusi vya Corona, tangu ulipozuka huko Wuhan, katikati mwa China. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Kama ishara, China, ambako ugonjwa huo ulianzia, ilitangaza Jumatano kuwa kikao cha kila mwaka cha Bunge, kitafunguliwa Mei 22.

Kikao hicho, ambacho kawaida huleta pamoja wabunge 3,000 katika jengo la makao makuu ya Bunge huko, Pekin, kitatoa nafasi kwa rais Xi Jinping kutangaza ushindi kwa nchi hiyo dhidi ya virusi vya Corona, wakati anaendelea kukosolewa kwa kuchelewa kutoa taarifa kwa ulimwengu kuhusu hatari ya maambukizi ya virusi vya Corona.

Watu milioni 3.1 duniani waliambukizwa virusi vya Corona, tangu ulipozuka huko Wuhan, katikati mwa China. Watu zaidi ya 217,000 wamefariki dunia, licha ya masharti ya watu kutotembea yaliyowekwa katika nchi nyingi duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.