Pata taarifa kuu
UN-USALAMA

Umoja wa Mataifa wahimiza nchi wanachama kutoa michango yao

Umoja wa Mataifa unatahadharisha nchi wanachama kuhusu kuchelewa kwa mchango katika bajeti ya shughuli za kulinda amani ulimwenguni.

Walinda amani wa Monusco wakipiga doria katika mitaa ya Goma, DRC, Machi 19, 2020.
Walinda amani wa Monusco wakipiga doria katika mitaa ya Goma, DRC, Machi 19, 2020. REUTERS/Olivia Acland
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Mataifa umezitaka nchi wanachama kutoa michango yao ili kulipia shughuli za kulinda amani za mwaka 2019.

Umoja wa Mataifa unaweza kupata usumbufu wa kulipa nchi zinazochangia kwa askari wa kikosi chake.

Baadhi ya shughuli za kulinda amani zimesitishwa hadi mwishoni mwa mwezi Juni.

Tangu janga la Covid-19 kuzorotesha shughuli katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa, tahadhari kadhaa zimechukuliwa ili kuhakikisha kuwa shughuli za kulinda amani zinaendelea bila usumbufu, au hata kusaidia katika nchi zinazo pambana dhidi ya Covid-19.

Ufaransa na Umoja wa Ulaya tayari zimetoa mfano mzuri kwa kusema mara moja kwamba hazitawarejesha nyumbani askari wao, wanao shiriki katika kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani. Canada, Uingereza na Uhispania walifikiria kwa muda fulani kuwarudisha nyumbani askari wao, lakini mwishowe waliachana na mpango wao.

Zaidi ya dola milioni 700 kutoka Marekani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataiaf, Antonio Guterres ametahadharisha nchi 193 wanachama wa umoja huo kuhusu hatari inayoweza kutokea kwa nchi hizi kukabiliwa na mgogoro wa ukwasi katika wakati huu mgumu.

Marekani tayari imelipa dola milioni 703, au nusu ya deni lake, kwa bajeti ya shughuli za kulinda amani, ambayo itawezesha Umoja wa Mataifa kulipa mishahara ya askari na polisi mwishoni mwa mwaka huu wa 2019 na kuendelea kujikwamu hadi miezi mitatu ijayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.