Pata taarifa kuu
ULAYA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Hatua za dharura kupunguzwa katika baadhi ya nchi za Ulaya

Baadhi ya nchi duniani zinataka kuanza kupunguza hatua za dharura kutokana na kudorora kwa uchumi kufuatia kukwama kwa shughuli nyingi kutokana na janga la Covid-19.

Baadhi ya nchi zinaelekea kuchukua hatua ya kupunguza hatua hizo kufuatia kudoroa kwa uchumi.
Baadhi ya nchi zinaelekea kuchukua hatua ya kupunguza hatua hizo kufuatia kudoroa kwa uchumi. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Hatua za dharura zilizochukuliwa na nchi kadhaa za Magharibi kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona zimeonekana kuzaa matunda jana Jumapili.

Hata hivyo baadhi ya nchi zinaelekea kuchukua hatua ya kupunguza hatua hizo kufuatia kudoroa kwa uchumi.

Ujerumani ambayo ni moja ya nchi za Ulaya inayotarajia kuanza kupunguza hatua hizo, inatarajia leo Jumatatu kuruhusu maduka kadhaa yanayopatikana kwenye umbali wa mita mraba 800 kufunguliwa.

Ulaya ina theluthi mbili ya vifo vya zaidi ya 164,000 vilivyotokana na janga la Covid-19 duniani.

Ujerumani ambayo ina visa zaidi ya 135,000 vya maambukizi vilivyothibitishwa na karibu vifo 4,000, imefaulu kudhibiti kwa kiwango kikubwa ugonjwa huo, " Waziri wa Afya Jens Spahn amesema.

"Mafanikio haya" bado ni "dhaifu", ameonya Kansela Angela Merkel, wakati Armin Laschet, kiongozi wa moja ya maeneo yaliyoathiriwa, North Rhine-Westphalia, ameonya kuwa "hatutaweza kuishi muda mrefu kama zamani.

Nchi kadhaa za Ulaya, ikiwa ni pamoja na Ufaransa (karibu vifo 20,000), Uhispania (karibu vifo 20,500) na Italia (zaidi ya vifo 23,600), zimethibitisha kupungua kwa idadi ya wagonjwa na vifo, baada ya wiki kadhaa idadi ya visa vya maambukizi na vifo kuongezeka; Nchi hizo inajiandaa kuchukuwa uamuzi wa kupunguza hatua za dharura.

"Hatujaondokana na mgogoro wa kiafya", hata kama "hali iinaboreka polepole, hatua kwa hatua", amebaini Waziri Mkuu wa Ufaransa Edouard Philippe, ambaye nchi yake, ya nne duniani iliyoathiriwa sana kwa vifo, baada ya Marekani, Italia na Uhispania, inajianda kupunguza hatua za dharura kuanzia Mei 11.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.